Ziara ya Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeendelea na ukaguzi wa Mradi wa Ukarabati wa Shule ya Msingi Sura iliyopo katika Kata ya Songoro.
Mradi huo umetumia takribani kiasi cha Shilingi Milioni 90 zilitengwa kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo fedha kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo fedha hizo zilipokelewa katika Shule ya Msingi Sura tarehe 22/01/2024 na taratibu za ukarabati zikaanza.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Felister Nanyaro amepongeza maendeleo ya zoezi hilo na kutoa wito kwa viongozi wa eneo hilo pamoja na walimu kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa wananchi ili wawe na uelewa wa kutosha kwa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Hata hivyo Mkuu wa shule ya Msingi Sura Godwin Emmanuel Mafie ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo na miradi mbalimbali kwani utasaidia Wanafunzi kusoma katika Mazingira bora zaidi.
Hadi sasa Mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 90 ambapo zoezi lililobaki ni hatua ya uwekaji wa Tailisi na kufanya usafi wa mwisho ambapo kazi hiyo ndiyo inayoendelea na Fedha iliyotumika mpaka sasa ni Shilingi Milioni 85.
Ukaguzi huo ni utaratibu wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa