Baraza la wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Meru lahimiza Halmashauri hiyo mbali na jitihada zilizofanyika za kuzingatia maslahi ya Watumishi katika maandalizi ya bajeti ya mwaka 2020/2021 kuhakikisha ina weka miundombinu rafiki kwa wafanyakazi wenye mahitaji maalum ili kuleta usawa mahala pa kazi.
Mwakilishi wa wafanyakazi wenye ulemavu Bibi.Vicky Kimaro amesema usawa kwa watumishi ni jambo muhimu hivyo Halmashauri haina budi kuboresha miundombinu rafiki kwa wafanyakazi wenye mahitaji maalum katika vituo vya kazi haswa vilivyopo pembezoni ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija.
Akitoa mfano Bibi Vicky amesema baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari hakuna vyoo kwa ajili ya Watumishi wenye mahitaji maalumu.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa baraza hilo Bi.Grace Mbilinyi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri itaendelea kuweka bajeti ya mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na miundombinu ya wafanyakazi wenye mahitaji maalumu.
Afisa Maendeleo ya Jamii kwenye Halmashauri hiyo Ndg.Hamson Mrema ametoa wito kwa walemavu kuchangamkia fursa ya mkopo kwa gharama nafuu unaotolewa na Halmashauri.
Mrema amesema mbali na Halmashauri hiyo kutenga bajeti kwa ajili ya mikopo kwa walemavu ni kikundi kimoja pekee cha watu wenye mahitaji maalumu kilichojitokeza kuomba mkopo Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kwa mwaka huu 2019/2020 hadi sasa ni vikundi Vinne pekee vimejitokeza.
Aidha Mrema amefafanua kuwa fedha za mikopo kwa gharama nafuu zinazotolewa kupitia mfuko wa Wanawake,vijana na walemavu kwa asilimia zinalenga kuwasaidia kuboresha shughuli za kiuchumi wanazofanya kwa kuwaongezea mtaji hivyo kigezo cha kuwa na shughuli ya kiuchumi kabla ya kupewa mkopo huzingatiwa.
Aidha viongozi toka vyama mbalimbali vya wafanyakazi ngazi ya Mkoa na Wilaya waliweza kuipitia bajeti hiyo na kutoa maoni yao ambapo Katibu wa TUGHE Mkoa wa Arusha Ndg. Samweli Magero ametoa rai kwa Halmashauri kuhakikisha maoni ya Baraza hilo na maboresho kuhusu maslahi ya watumishi yaliyotolewa kuzingatiwa kabla bajeti hiyo haijaenda hatua nyingine.
Mwakilishi wa walimu kutoka Shule ya Sekondari Makiba Mwl. Vistus Sylidion ameipongeza Halmashauri kwa kufuata sheria kuhakikisha wafanyakazi wanashiriki kikamilifu katika mchakato wa bajeti.
Mkutano huo maalumu wa baraza la wafanyakazi kujadili bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikisha wafanyakazi wote kutoka Idara 14 na Vitengo 6 vya Halmashauri pamoja na viongozi kutoka vyama vya wafanyakazi TUGHE, CWT, TALGU, TTU, RAAWU
Mwenyekiti wa Baraza ka wafanyakazi Bi.Grace Mbilinyi akizungumza.
Mwakilishi wa wafanyakazi wenye Ulemavu Wilaya ya Arumeru Bibi Vicky Kimaro akitoa maoni juu ya miundombinu rafiki.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa Baraza.
Katibu wa CWT Mkoa wa Arusha Ndg.Felix Mnyanyi akihoji kiwango cha posho kwa watumishi.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa Baraza.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Arusha Ndg. Samweli Magero akizungumza .
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa Baraza.
Katibu wa CWT Wilaya ya Arumeru akizungumza.
Katibu wa baraza la wafanyakazi Oliver Swaty na kushoto ni katibu msaidizi Charles Mungure
Katibu wa TALGU Mkoa wa Arusha Ndg.Jonathan Ndumbaro akizungumza.
Mapitio ya Bajeti ya Halmashauri.
Kulia ni Katibu wa RAAWU Mkoa wa Arusha akichambua bajeti
Mapitio ya Bajeti .
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa Baraza.
Tovuti yetu .www.merudc.go.tz
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa