Wananchi katika Halmashauri ya Meru wajitokeza kwa Wingi kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo kwa Halmashauri ya hiyo iliadhimishwa kwa kutoa huduma kwa wananchi bila malipo za upimaji virusi vya UKIMWI (VVU) ,Uchunguzi wa kifua kikuu na huduma ya Afya ya Uzazi wa mpango ,huduma hizi zilitolewa kwenye maeneo ya Kikatiti,Usa-River na Tengeru.
Maadhimisho hayo kwa Halmashauri hiyo kupitia Idara yake ya Afya yalianza kuanzia Tarehe 24 Novemba 2017 hadi Tarehe Mosi Disemba kwa kupima VVU ili kuwatambua wenye maambukizi na kuwaunganisha kwenye huduma za matibabu ambapo jumla ya watu 1004 ,wanaume wakiwa 363 na Wanawake 641 walipima Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU)
Aidha Tarehe Mosi Disemba kila mwaka ni killele cha Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani hili ni kutokana na mnamo 1981 tarehe Moja Disemba ndiyo siku ambayo Kirusi cha UKIMWI kilitambulika rasmi Duniani.kwa mwaka huu katika siku hii ya maadhimisho ya UKIMWI Duniani kwa Halmashauri ya Meru Jumla ya watu 475 walipima VVU
Akizungumza wakati Maadhimisho hayo Daktari.Wicklif S. Sango ambaye ni mratibu wa UKIMWI wilaya ameeleza umuhimu wa kupima Afya unamwezesha mtu anapojikuta hana maambukizi anafanya maamuzi ya kujiweka salama na kwa atakaye jikuta tayari anamaambukizi itamwezesha kuanza matibabu mapema na kuishi maisha ya Afya yatakayo mwepusha na magonjwa nyemelezi.
Upimaji huu ulifanyika kwa watu wazima pamoja na watoto wenye Umri kuanzia mwaka mmoja.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa