• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

BIMA ZA ICHF ZATOLEWA KWA WANAFUNZI 105 WENYE MAHITAJI MAALUM.

Imewekwa: March 4th, 2021


Timu ya uendeshaji huduma za afya (CHMT) Halmashauri ya Wilaya ya Meru, yagawa kadi za mfuko wa afya wa jamii ulioboreshwa (ICHF) kwa watoto 105 wenye mahitaji maalumu katika shule ya Msingi patandi maalum iliyopo katika Halmashauri hiyo

Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus amesema timu hiyo imewakatia  bima hizo wanafunzi  kama sehemu ya upendo kwa , kuboresha mahusiano na jamii sambamba na kuhamasisha  jamii kujiunga na bima ya ICHF ili kuweza kupata matibabu  kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa gharama yaelfu 30 tu.

Maneno amesema timu hiyo ya  kwa kutambua umuhimu wa matibabu wakati wote inahamasisha Kaya elfu 58 ambazo hazitumii bima yoyote  kujiunga na ICHF ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu muda wote kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa gharama ya shilingi elfu 30.

Mratibu wa ICHF Wilaya Ndg.Adalbet Temba  amesema   bima ya  ICHF yenye gharama ya shilingi elfu 30  inatumika kulipia gharama za huduma zote za msingi ikiwa ni kumwona daktari,dawa na  vipimo vya msingi ambapo ametoa wito kwa jamii kujiunga na bima hiyo .

Temba amesema mwananchi anaweza kujiunga na   ICHF kwa kufika ofisi ya mtendaji wa kijiji ili kuunganishwa na afisa mwandikishaji ambapo atapaswa kulipa shilingi elfu 30  ikiwa ni bima kwa wanakaya 6 yaanimkuu wa kaya mwenza na wategemezi 4 ambao watapata huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati ,Kituo cha afya,Hospitali ya Wilaya na hospitali za rufaa .

Temba amehitimisha kwa kufafanua kuwa bima ya ICHF itatumika kwakuzingatia rufaa, yani mwanachi atapaswa kutibiwa kuanzia ngazi ya Zahanati,Kituo cha afya,Hospitali ya Wilaya na hospitali ya rufaa ya Mkoa .

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya  Mwl.Marcus Nazi, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi amepongeza timu ya CHMT Pia ametoa wito kwa wazazi wenye wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kuungana kuwakatiawanafunzi hao bima za ICHF ili kuwa nauhakika wa matibabu wakati wowote“Wanafunzi 5 wanaweza kupata bima ya ICHF kwa kipindi cha mwaka mmoja kwagharama ya shilingi elfu 30 tu “amesisitiza Mwalimu Nazi.

Mwl. Jackline Mtui ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Patandi maalum ameishukuru kamati ya CHMT kwa kuwakatia wanafunzi 105 wenye ulemavu shuleni hapo ambao wanachangamoto ya akili,Usonji,wasioona na viziwi.


Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya  Mwl.Marcus Nazi, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, akizungumza wakati wa hafla fupi  ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.

Mganga Mkuu wa Halmashaurhi hiyo Dkt.Maneno Focus akizungumza wakati wa hafla fupi  ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.

Mratibu wa ICHF Halmashauri ya Wilaya ya Meru  Ndg. Adalbet Temba akizungumza wakati wa hafla fupi  ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum.

Mwl.Jackline Mtui ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Patandi maalum  akizungumza wakati wa hafla fupi  ya kukabidhi bima za ICHF kwa Wanafunzi105 wenye mahitaji maalum. 

Wanafunzi wa SHule ya Msingi Patandi maalum walionufaika na bima za ICHF

Mwl. Marcus Nazi akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kadi ya ICHF zilizotolewa na timu ya HMCT Halmashauri ya Meru.

Naomi ni  miongoni mwa wanafunzi 105 wanufaika wa bima za afya ICHF zilizotolewa na timu ya HMCT Halmashauri ya Meru.

Miongoni mwa Wanufaika wa bima za afya ICHF zilizotolewa na timu ya HMCT Halmashauri ya Meru.

Mkuu wa shule ya Msingi Patandi Maalum Mwl. Jackline Mtui akipokea zawadi za wanafunzi toka kwa mgeni rasmi.

Picha ya pamoja ya Meza kuu na Wanafunzi wa shule ya Msingi Patandi maalumu.

Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa hafla ya kukabidhi bima za ICHF kwa wanafunzi 105

Picha ya pamoja mgeni rasmi,Walimu wa shule ya patandi Maalum na timu ya HMCT Wilaya.

Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru


Wajumbe wa kamati ya HMCT Halmashauri ya Wilaya ya Meru


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa