Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Madiira wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule nzuri katika Kata ya Seela Sing'isi.
Akiwakilisha wanafunzi wenzake Glory Kaaya amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul C. Makonda kufika shukrani hizo na salamu zao kwa Mhe. Rais Samia.
Aidha, wanafunzi hao wamewasilisha ombi lao kwa Mhe. Rais Samia la kujengewa Mabweni na Nyumba za Walimu ili kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu na kuwa karibu na walimu wakati wote ili kuendelea kuboresha mazingira ya kusoma.
Ikumbukwe kuwa shule Mpya ya Sekondari ya Madiira iliyopo Kata ya Seela Sing'isi inahudumia wanafunzi wanaotoka Kata ya Poli, Akheri, Seela Sing'isi na Kata nyingine za jirani.
Pia, Shule hiyo imejengwa kwenye eneo la Halmashauri lenye ukubwa wa ekari 12.5 ambapo miundombinu iliyojengwa ni pamoja na majengo ya madarasa, Jengo la Utawala,maabara ya kemia, fizikia na baiolojia, Jengo la Tehama, Maktaba pamoja na vyoo vya jinsia zote, kichomea taka na taki la maji safi la ardhini.
https://www.instagram.com/reel/C7l4_DQtJhx/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA== Fungua hapa kupata taarifa hii.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa