Wanafunzi wa Shule ya Msingi Precious English Medium wakifanya onesho maalumu linalotoa elimu juu ya Malezi mema katika familia.
Katika onesho hilo limeonesha familia mbili, moja ya wazazi walioshikamana na kulea mtoto katika maadili mema na ya pili ni familia ya wazazi wanaolea watoto kwa shida na mfarakano unaopelekea mtoto kukosa amani na mshikamano na matokeo yake mtoto kushindwa kufanya vyema Darasani
Maonesho hayo yamefanyika Mei 15, 2024 Shule ya Precious English Medium katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia.
Kauli mbiu katika maadhimisho haya ni " Tukubali Tofauti Zetu kwenye Familia, Kuimarisha Malezi ya Watoto"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa