Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs C. M. Mwambegele na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 29 Novemba, 2024 amekutana na Wadau wa Uchaguzi katika Mkutano wa Tume hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Lengo la Mkutano huo ni kuanza maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mwaka 2024 kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025 ambapo jumla ya wapiga kura wapya 224,499 wanatarajiwa kuandikishwa Mkoani Arusha.
Mhe. Jaji (Rufaa) Mwambegele ameeleza kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Tume imepewa Mamlaka ya kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara.
Aidha, ameeleza kuwa zoezi hili lilishaanza kwa baadhi ya maeneo na Mikoa kama vile Geita, Kagera, Kigoma, Tabora, Katavi, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu Manyara,Dodoma,Singida na Zanzibar lakini kwa sasa Tume inafanya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la kudumu kwa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mkoa wa Dodoma kwenye Halmashauri za Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa kuanzia tarehe 11 Desemba, 2024 hadi tarehe 17 Desemba, 2024.
Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura utahusisha matumizi ya teknolojia ya Biometric Voters' Registration BVR ambao hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine kwa kuwa unahusisha uchukuaji wa alama za vidole vya mikono, picha na saini na kuhifadhiwa kwenye kanzidata ya wapiga kura.
Wadau walioshiriki katika Mkutano huo pamoja na Vyama vya Siasa vyenye Usajili, Viongozi wa Dini na Asasi za Kiraia, Taasisi, Makundi mbalimbali ya Vijana, Wanawake, watu wenye Ulemavu, Wahariri, Waandishi wa Habari na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri katika Mkoa wa Arusha.
Mhe. Mwambegele katika Mkutano huo ameambatana na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima, R. K na Mhe. Dkt. Zakia Abubakar Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa