Wananchi wa Manyata Wilayani Arumeru wapongeza utendaji wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jerry Muro ambao unalenga kutatua kero za wananchi na kuwaletea Maendeleo.
Hayo yameelezwa na wananchi hao wakati wa uzinduzi Mradi wa TASAF wenye thamani ya Tsh.64,919,458.01 wa kukarabati barabara ya Manyata - Nganana urefu wa Km 5.7, ambapo mkuu huyo wa Wilaya alikuwa mgeni rasmi.
Aidha baada ya uzinduzi wa mradi huo ambao kwa mujibu wa utekelezaji wa TASAF unatambua Manyata kama kijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru chenye vitongoji viwili Manyata kati na Nganana Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alitoa fursa kwa wananchi hao kutoa kero zao ambazo zilitatuliwa papo kwa papo na nyingine kuchukuliwa kufanyiwa kazi na wananchi watapewa mrejesho mapema.
Mmoja wa wanakijiji wa Manyata mama vumilia ambaye ni mlengwa wa TASAF amempongeza Mkuu wa wilaya kwa kutatua kero zilizokua zinawakabili pamoja na hatua alizochukua za kumaliza kero kubwa ya Maji ampapo wakilishi 10 wa wananchi watahudhuria kikao cha utatuzi wa kero hiyo kitakachofanyika ndani ya siku 7, "Mkuu wa Wilaya tumefurahi sana kwa ujio wako katika kijiji chetu kwani wananchi wa Manyata kwa muda mrefu hatujawahi pata fursa ya kutembelewa na Mkuu wa Wilaya kwaajili ya kusikiliza shida tulizonazo hivyo tunamshukuru Mhe.Rais kukuleta katika wilaya hii " ameeleza vumilia .
Wananchi hao wa Manyata wamemzawadia Mhe.Jerry Muro mbuzi na kumvisha vazi la heshima .
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru amekuwa mbunifu kwa kutumia mbinu mbalimbali kwenye utatuzi wa kero za wananchi katika Wilaya hiyo ambapo hivi karibuni aliendesha zoezi la kusikiliza kero za wananchi lilipewa jina la PAPO KWA PAPO likiwa na maana ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maamuzi ya haraka kwa mijibu wa sheria.
Serikali kupitia mfuko wa TASAF imeidhinisha kiasi cha Tsh.64,919,458.01 kwaajili ya ukarabati wa barabara ya Manyata - Nganana km 5.7.
Ikumbukwe Kwa sasa Manyata ni miongoni mwa vitongoji vinavyounda Mamlaka ya Mji mdogo Usa - River
Afisa mwendeshaji wa Mamlaka ya Mji mdogo Usa - River Monica Kimario akikabidhi zawadi iliyotolewa na Wananchi wa kijiji cha Manyata ya mbuzi mme kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Moro.
Mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Manyata wakati wa uzinduzi wa mradi wa kukarabati barabara ya Manyata - Nganana.
Wananchi wa kijiji cha Manyata wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata -Nganana.
Wananchi wa kijiji cha Manyata wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata -Nganana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa