Wananchi wa Halmashauri ya Meru ,Wilayani Arumeru waipongeza Serikali ya Awamu ya tano kwa uboreshaji wa huduma za Afya Wilayani humo.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wananchi hao wameishukuru Serikali kwa kutenga Milioni 500 za ujenzi wa jengo la upasuaji, Wodi ya Mama na mtoto, Maabara, Nyumba ya Mtumishi, Jengo la kuhifadhia Maiti na Kichomea Taka na kukarabati miundombinu iliyokuwepo katika kituo cha Afya Usa - River. "sisi kinamama tumenufaika sana, tunajifungulia sehemu nzuri na karibu"ameeleza Neema Shao mkazi wa Usa River.
Eliuwoo Mbise ambaye ni mama wa mtoto mgonjwa , ameishukuru Serikali kwa uboreshaji wa kituo cha Afya Usa - River kwani awali walitumia gharama kubwa ya usafiri kufuata matibabu katika Hospitali ya Wilaya, pia walitumia muda mwingi wanapofika Hospitali ya Wilaya kutokana na msongamano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ,Ndg. Emmanuel Mkongo ametoa wito kwa watumishi wa Afya kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kutoa huduma zenye tija " hakikisheni lengo la Serikali la Wananchi kupata huduma za afya zenye ubora unaostahiki karibu na maeneo wanayoishi linatimia” amesisitiza Mkongo
Aidha Kituo cha Afya Usa – River ni miongoni mwa vituo vya Afya 352 vitakavyo zinduliwa na Mhe.Rais kesho katika Halmashauri ya Mji wa Masasi Mkoani Mtwara ambapo Kituo cha afya cha Mbonde kitazinduliwa kwa niaba ya vituo vyote 352 Nchini.
Eliuwoo Mbise (wa kwaza Dirishani) ambaye ni mama wa mtoto mgonjwa akipata huduma alipowasili kituo cha Afya Usa River.
Neema Shao akielezea kwa furaha kinamama walivyonufaika na Uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa - River.
Muonekano wa Mbele wa kituo cha Afya Usa - River.
Jengo la upasuaji Kituo cha Afya Usa - River.
wodi ya Mama na Mtoto Kituo cha Afya Usa - River.
Jengo la Maabara katika cha Afya Usa - River.
nyumba ya mtumishi Kituo cha Afya Usa - River.
Chumba cha kuifadhia maiti Kituo cha Afya Usa - River.
Kichomea taka
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa