Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewataka wananchi wa Wilaya hiyo waliojenga kwenye mikondo ya asili ya maji kupisha mikondo hiyo kuepuka madhara ya mafuriko.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua athari zilizotokana na mafuriko Kata ya Ambureni Halmashauri ya Meru, Muro amewataka wananchi kuepuka madhara ya mvua zinazoendelea kwa kuondoa makazi kwenye mikondo ya maji."ili muwe salama lazima mkae pahala salama hivyo wote waliokwenye mikondo ya maji pisheni mikondo hiyo"amesema Muro
Mhanga wa mafuriko hayo Modesta Isaya ambaye pia ni mwalimu wa shule ya msingi Wilayani humo ameiomba Serikali na wadau wamsaidie kupata makazi mapya kwani nyumba yake ya vyumba 6 ipo kwenye mkondo wa maji hivyo anatakiwa kuhama , ”mimi ni mama wa familia ya watoto 4 nipo tayari kuhama hapa ila sina pakwenda naiomba Serikali na wadau mbalimbali wanisaidie kupata makazi mapya”amesema Modesta.
Mtendaji wa Kata ya Ambureni Ndg.Philipo J Philipo amesema uongozi wa kata hiyo umemtafutia sehemu ya hifadhi Modesta pia kwa kushirikiana na wadau inafanya juhudi za kukarabati miundombinu iliyoathiriwa ikiwemo barabara ya Kwapole sambamba na kusimamia agizo la Mkuu wa Wilaya la kuwataka wananchi walio kwenye mikondo ya maji wanakua salama kwa kuhama.
Mratibu wa Maafa Halmashauri ya Meru Digna Masawe ametoa wito kwa Wananchi wa Halmashauri hiyo kuchukua tahadhari za kukabiliana na maafa kwa kuzibua mifereji,kuhama mabondeni pamoja na kuondoa makazi kwenye mikondo ya maji
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa