• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

WANANCHI MERU WATUMA SALAMU KWA MHE.RAIS

Imewekwa: June 1st, 2023

Wananchi wa Kijjiji cha Kaloleni  Kata ya Majengo Halmashauri  ya Wilaya ya Meru,  Wilayani Arumeru wamemshukuru Dkt.Samia  Suluhu  Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kutoa Milioni 106.3 za ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa  na vyoo vya  wanafunzi  wa kike matundu manne.

Wananchi wamesema hayo wakati wa ziara ya  Mkuu wa Wilaya  ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda ya kukagua utekezaji wa miradi ya BOOST katika Halmashauri  ya Wilaya ya Meru.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kaloleni  Diwani  wa Kata ya Majengo Mhe.Bernard Kivondo amemshukuru Rais.Samia kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo katika  shule ya Msingi Kaloleni kwa awamu ambapo Serikali kupitia TASAF ilitoa milioni 74 za ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa na ofisi, pia ilitoa milioni 12.5 za ukamilishaji wa boma na sasa imetoa Milioni 106.3 fedha za mradi wa BOOST  kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa  na vyoo .

Aidha, Mhe.Kivondo amesema Wananchi wa Kaloleni wamehamasika na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Dkt.Samia Suluhu  Hassan  na  wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi kwa kuchangia nguvu kazi ambapo vitongoji vya kijiji cha Kaloleni vinautaratibu wa  zamu ya nguvu kazi.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela  Kaganda  amesema Serikali  ya  Dkt.Samia  Suluhu  Hassan  imejipanga  kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa ngazi zote ambapo katika sekta ya elimu msingi imetoa milioni 961.5 fedha za BOOST  kwa ajili ya  uboreshaji wa miundombinu katika shule za msingi ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.

Aidha, Mhe.Kaganda  ameelekeza  miradi inayotekelezwa  kuwa na viwango na ubora sambamba na kutekelezwa kwa wakati .

 *Ikumbukwe*

Ilani ya CCM ya mwaka 2020, Sura ya tatu  ibara ya 78 inaeleza "CCM inatambua kuwa rasilimaliwatu ndio nyenzo muhimu ya maendeleo  ya kijamii na kiuchumi. Aidha CCM inaamini kuwa elimu bora ndio nyenzo muhimu ya kujenga ,kulea na kuendeleza rasilimaliwatu ili ziweze kuchangia  kikamilifu katika ujenzi  wa Taifa  na maendeleo  ya jamii kwa ujumla"


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa