Leo tarehe 16 Oktoba 2024, Wajumbe wawili wa Kamati ya Hamasa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Daniel Nanyaro na Annamaria Makweba Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msimamizi Msaidizi Wa Uchaguzi wamefika katika kituo cha utangazaji cha Redio Safina kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Pamoja na kuelezea sifa mbalimbali za Mgombea na mpiga kura , pia wameeleza tofauti kati ya uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi linaloendelea la kujiandikisha kwenye daftari la wakazi la wapiga kura.
Enezael Elia Leboi ni Mtangazaji wa Radio Safina ameendesha kipindi hicho kinachohusiana na masuala ya Uchaguzi wa Serikali za Mita
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa