Wananchi wa kijiji cha Maroroni kilichopo Kata ya Maroroni Halmashauri ya Meru wamepokea na kuridhia Mradi mpya wa usambazaji Maji kijijini hapo kwa furaha kubwa,haya yamejiri kwenye mkutano wa wanakijiji hao uliohudhuriwa na wataalamu toka Halmashauri ya Meru na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kwa lengo la kutambulisha Mradi mpya wa usambazaji Maji kijijini hapo utakao wezesha upatikanaji wa Maji kua umbali wa Mita 400 tu .
Akitoa elimu ya Miradi ya Maji Happyness Mrisho ambaye ni Mhandisi wa Maji wa Halmashauri hiyo ameeleza Sera ya Maji ya mwaka 2002 inaelekeza Jamii kushiriki katika kuibua, kupanga na kutekeleza Miradi ya Maji jambo ambalo ofisi yake inalizingatia na kuwasihii wananchi kua huru kutoa maoni yao juu ya Mradi huo ili uwe wa manufaa kwao .
Wananchi walipokea mradi huo na kushauri mambo mbalimbali yazingatiwe, mwanakijiji aliyetambulishwa kwa jina la Isaya alishauri Jeografia ya kijiji hicho ipitiwe ili watu wote waweze kupata maji jambo lililopelekea Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Christopher Kazeri kumwagiza Mhandisi huyo kuhakikisha anawashirikisha wananchi kila hatua ya mradi huo pamoja na kuwapa mrejesho kwa kila hatua.Naye katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava amepokea Malalamiko ya baadhi ya wananchi juu ya upatikanaji maji katika kijiji jirani cha Samaria kwa kueleza kua wananchi wa Samaria ni wa Arumeru na wanahitaji maji pia hivyo wanalichukua hilo na kulifanyia kazi.
Aidha Wanakijiji wa Kijiji cha Maroroni wanapata Maji kupitia Mradi wa maji wa KIMASIKI unaohudumia vijiji vipatavyo ambavyo ni Kikatiti,Maroroni,Samaria na Kitefu jambo Linalosababisha wananchi hawa kupata maji kidogo kwenye umbali mrefu .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa