Wananchi wa Kijiji cha Maji ya Chai Halmashauri ya Meru wakiwa kwenye mkutano wa kijiji wamepokea Uibuaji wa Mradi Mpaya wa usambazaji Maji kijijini hapo utakao tekelezwa kwenye vitongoji 3 Maji ya Chai Center,Kimandafu na K.center na kuomba mradi huo kuanza kutekelezwa mapema kwani upatikanaji wa maji kwao umekua changamoto waliyoifananisha na kilio,
Pia wanachi hao wameridhia kuunganishwa kwenye Mamlaka ya Maji Usa -River ili kulipia huduma ya Maji itakayowawezesha kupata maji kila siku tofauti na sasa ambapo upatikanaji wa maji si wa uhakika pia ni mdogo jambo ambalo ni kero kubwa kwao,
Akieleza manufaa ya kupata huduma ya maji kupitia Mamlaka ya Mji mdogo Usa-River Meneja mwendeshaji wa mamlaka hiyo Mhandisi Antidius Mchunguzi amesema Mamlaka hiyo itawaezesha wananchi hao kupata Huduma ya maji ya uhakika yaani kila siku, na kupunguza gharama za kununua Maji sh 500 kwa(dumu) lita20 waliyokiri kulipia ambayo ni kubwa sana ukilinganisha na itakayotozwa na mamlaka hiyo sh 6, akisistiza ulipaji nafuu wa tozo za maji kwa msemo wa "Tozo za maji sio biashara" .
Naye Mhandisi wa Maji Happy Mrisho amesema kuwa Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania unazingatia lengo la serikali la kutaka wananchi Kusimamia, Kuipenda na kuthamini Miradi ya Maji katika Maeneo yao hii ni kwa mujibu wa Sheria namba 12 ya huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Christopher J.Kazeri amewataka wananchi hao kuchagua wajumbe wa kamati watakao kua na uelewa mpana wa maeneo ya kijiji hicho jamba ambalo litakua msaada kwa wataalamu wa idara ya maji wakati wa kufanya uchunguzi wa awali wa mradi huu pia amewaasa kutokuchagua wajumbe hao kisiasa .
Akizungumza kwa niaba ya wanawake Ndeterivio S. Sumari ambaye ni mama wa familia kutoka Kitongoji cha Kimandafu ameishukuru Halmashauri ya Meru kwa Kupeleka Mradi huu utakao waondolea kinamama adha ya upatikanaji wa Huduma ya Maji ikiwa ni kupoteza muda mwingi wa kuchota maji umbali mrefu tena maji kidogo
Ndeterivio S. Sumari akizungumza kwa niaba ya wanawake kwenye Mkutano wa wanakijiji wa Maji ya Chai.
Meneja mwendeshaji wa Mamlaka ya Maji Usa-River Mhandisi Antidius Mchunguzi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa