Wananchi wa Kijiji cha Mikungani Kata ya Mbuguni waondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama baada ya Shirika lisilo la kiserikali la WAMATA kuchimba kisima cha maji kilichogharimu Milioni 79.98 chenye urefu wa mita 130 kinachotumia nishati ya umeme wa jua.
Akizungumza katika makabidhiano ya Mradi huu ,Diwani wa Kata ya Mbuguni Mhe.Laurence Ngolly ametoa wito kwa wananchi kutunza mradi huo ili kuwa na manufaa kwa jamii ya sasa na badae ambapo ameweka bayana Uongozi wa Kata hiyo kutomvumilia yeyote atakayejaribu kwa namna yeyote kuhujumu mradi huo " nitoe wito kwa kila mwananchi kuwa mlinzi wa mradi huu wenye manufaakwetu sote"amehimiza Mhe.Ngolly
Mkurugenzi shirika hilo la WAMATA Bw. John Tarimo amesema wakati wa utafiti ilionekana Kijiji cha Mikungani kinachangamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama hivyo kutokana na Sera na ushirikiano uliopo kati ya Serikali na wadau wameweza kuchimba kisima ambacho kitahudumia zaanati ,shule na wananchi ambao wamewekewa vilula 2 vya maji(DP).
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru ambaye pia ni mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti taka B. Charles Mboya ametoa wito kwa jamii kutunza vyanzo vya maji sambamba na kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti wananchi hao wameshukuru kupata mradi huo kwani upatiksnaji wa maji ulikuwa changamoto kubwa "tulikuwa tunanunua maji lita 20 Shilingi elfu moja na kutokana na kipato cha wengi wetu kuwa chini tulikua tukifuata maji kwenye visima vya mashambani"amesema Perpetua Mafie Mkazi wa Kijiji cha Migungani
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Meru inawakaribisha na itaendelea kushirikia na wadau mbalimbali kuwaletea wananchi maendeleo .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa