Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameshauriwa kupata huduma bora na zenye uhakika zinazotolewa na Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya na zahanati za Serikali zilizopo .Ushauri huo ameutoa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho alipozindua jengo la kinywa na meno katika Hospitali ya Wilaya ya Meru(Tengeru).
Aidha Ndg.Kabeho amesema ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo pamoja na mashine zilizopo zinatosha kutoa huduma hivyo jamii haina budi kunufaika na huduma za afya ya kinywa na meno katika Hospitali hiyo.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Cosmas Kilasara amesema huduma zinazotolewa kwenye jengo hilo ni usafishaji wa meno, uwekaji wa meno bandia, uzibaji wa meno yaliyotoboka pamoja na Ung'oaji wa meno .
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la kinywa na meno katika Hospitali ya Wilaya Tengeru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akiweka jiwe la uzinduzi katika jengo la kinywa na meno katika Hospitali ya Wilaya Tengeru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho baada ya kuweka jiwe la uzinduzi katika jengo la kinywa na meno katika Hospitali ya Wilaya Tengeru.
Watumishi wa Idara ya Afya wakishangilia uwekaji jiwe la Uzinduzi katika jengo la kinywa na meno katika Hospitali ya Wilaya Tengeru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa