Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg. Emmanuel J. Mkongo ametoa wito kwa wananchi Jimboni humo kujitokeza kwa wingi siku ya Kesho , tarehe 28 Octoba 2020 ikiwa ni siku ya uchaguzi Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi kwa kuwapigia Kura .
Akizungumza ofisini kwake ,Mkongo amesema maandalizi ya Uchaguzi huo jimboni humo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kubandika orodha ya wapiga kura waliojiandikisha katika vituo vyote 521 pamoja na kuwajengea uwezo Makarani waongozaji na Wasimamizi wa vituo hivyo vya kupigia kura.
Mkongo amesema Vituo vya kupigia Kura vitafunguliwa Saa 1:00 kamili asubuhi na Kufungwa Saa 10:00 kamili jioni, hivyo amewataka wanachi kuwahi kupiga kura na kurudi nyumbani kusubiri matokeo.
Aidha Mkongo, amefafanua kuwa Wananchi walio poteza kadi zao za kupiga kura wanaweza kupiga kura kwa kutumia vitambulisho mbadala ambavyo ni leseni ya Udereva, hati ya kusafiria na kitambulisho cha utaifa kinachotolewa na NIDA .
Akihitimisha ,Mkongo ametoa Wito kwa Jamii kudumisha amani iliyopo "busara kwa Wananchi ni kupiga kura na kwenda nyumbani kusubiri matokeo " amesisitiza Mkongo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa