Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Fautine Ndugulile awataka watumishi wa Afya kwenye Halmashauri ya Meru kutekeleza majukumu yao kuendana na kasi ya Mhe. Raisi wa awamu ya tano John Joseph Magufuli, hayo ameieleza timu ya uendeshaji wa huduma za afya katika Hopitali ya wilaya ya Halmahauri hiyo alipokua kwenye ziara yake ya siku moja yenye lengo la kuangalia hali ya upatikanaji wa dawa na kujiridhisha na utoaji wa uduma za afya.
Aidha Naibu waziri huyo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa matumizi mazuri ya fedha kwani imeweza kuboreha na kufanya upanuzi wa majengo ya wodi ya kina mama wajawazito, jengo la huduma ya Meno (Dental Unity) na jengo la utawala pongezi hizi amezito sambamba na kufanya vizuri kwenye utoaji wa chanjo,usafi unaoridhisha kwenye Hospitali hiyo ya Wiaya na utoaji wa huduma za afya jambo ambalo amejiridhisha baada ya kutembelea maeneo kadha ya kutolea huduma kwenye hospitali hiyo na kuwahoji wagonjwa namna wanavyohudumiwa .
Naibu Waziri amesema Serikali imeongeza bajeti ya Dawa kwa asilimia 80 kutoka kiasi cha bilioni 30 hadi bilioni 261 hivyo hategemei mwananchi kukosa dawa kwenye vituo vya kutoa huduma za Afya na kuviagiza vituo hivyo kuhakikisha vinaagiza dawa zote zinazohitajika pia katika kudhibiti matumizi ya dawa hizo ujazaji wa fomu za huduma za dawa (BIN GARD) ufanyike .
Katika kutatua changamoto zilizopo kwenye Idara hiyo ya Afya ameshauri ni vema kukawa namipango mikakati ya kukabiliana na vifo vya mama na mtoto,magonjwa yasiyoambukiza kwani yameshamiri kwa sasa na uzazi wa mpango ,Naibu huyo amemtaka meneja wa MSD Kanda ya Kaskazini Billy Singano, kutembelea mara kwa mara Hospitali ili kujua changamoto za upatikanaji wa dawa na kuzifanyia kazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za Afya .
Akizumngumza na Wananchi waliokua wameudhuria matembezi shirikishi(Site walk through) yaliyofanyika kwenye kituo cha Afya Mbuguni yakifadhiliwa na shirika la Engender Health kwenye Mradi wa LAD kwa lengo la jamii hiyo kutembelea kituo hicho cha Afya na kuibua changamoto zilizopo pamoja na kuzitatua zile zinazowezekana kwa ngazi yao ambapo wananchi hao wameweza kutatua changamoto ya chumba cha kuhifadhia chanjo kuvuja na kutokua kwenye hali nzuri kwa kuchangia bati 6 na mbao pamoja changamoto ya upungufu wa viti kwa kuchangi Fedha sh 205,000 na viti 6,huku wakichukua baadhi ya changamoto zilizo baki na kuhaidi kuzifanyia kazi ikiwemo upatikanaji wa maji, Amewataka wananchi hao kua mstari wa mbele kwenye kudhibiti matumizi mabaya ya dawa kwa kuhakikisha wawakilishi wao waliopo kwenye bodi wanakwepo wakati wa mapokezi ya dawa.Pia amewata wananchi hao kushiriki shughulli za maeneleo ikiwemo kutat.ua changamoto ndogondogo zilizopo kwenye kituo hicho, na kuliponeza Shirika lililoandaa matembezi haya, naye Sebastani Macrice kutoka shirika hilo la Engender Health ambaye ni Afisa mradi huo wa LDA amesema matembezi hayo shirikishi ni sehemu pia ya jamii hiyo kupata elimu juu ya huduma zinazopatikana katika kituo hicho ,elimu juu ya uzazi wa mpango pamoja na Huduma ya mama mjamzito ambaye mimba itaharibika kusafishiwa Hospitali.
Naye mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Cosmas Kilasara ametatu changamoto ya gari la kubebea wagonjwa lililodaiwa na wananchi kama changamoto kubwa kwakua umbali kutoka kituo hicho hadi Hospitali ya Wilaya nizaidi ya Kilometa 30 kwa kuhaidi kituo hicho kitapewa gari hilo hivi karibuni.
Sebastiani Macrice kutoka shirika la Engender Health ambaye ni Afisa Mradi wa LAD akieleza umuhimu wa matembezi shirkishi
Kushoto ni Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Fautine Ndugulile akisalimiana na Mganga Mkuu wa Hamashauri ya Meru Cosmas Kilasara alipowasili kwenyenye Hospitali hiyo ya Wilaya kwaajili ya ziara ya siku moja.
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Fautine Ndugulile akiwauliza kinamama waliohudhuria waliowaleta watoto wao kliniki katika kituo cha afya Usa-River namna huduma zinavyotolewa kituoni hapo.
Kulia ni Mkurugenzi wa MSD Taifa Victoria Elangwa ,Kushoto kwake ni Meneja wa MSD kanda ya Kaskazini Billy Singano
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa