Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru watakiwa kushirikiana ili kunyanyuana kiuchumi na kuharakisha maendeleo.
Wito huo umetolewa na Julieth Maturo mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) Wilaya ya kichama ya Meru wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Julieth amesema ni wakati wa wanawake kuinuana na kushirikiana kikamilifu kufuta dhana potovu ya adui wa mwanamke ni mwanamke "wanawake tushikane mikono tuinuane,tupendane kwa maendeleo yetu na taifa"amesisitiza Maturo.
Aidha, Maturo amempongeza Mhe.Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwathamini na kuwapa nafasi wanawake kwani wameweza kujiamini na kufanya vizuri zaidi "tunajivunia katika Nchi yetu Wanawake wamepewa nafasi za juu na kufanya vizuri, Mhe. Makamu wa Rais ni mwanamke,tuna Mawazari wanawake, Wakuu wa Wilaya na hata Wakuu wa Idara wa Halmashauri yetu na wote hao wamekua wakifanya vizuri."amesema julieth
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bi.Furahisha Magubila amesema wameungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa kufanya maandamano ya amani, kutoa msaada katika kituo cha wazee kilichopo kikatiti. Pamoja na kuelimishana juu ya ujasiriamali,lishe ,huduma za kibenki na maswala ya unyanyasaji wa kijinsia.
Kwa upande meneja wa kituo cha kulelea wazee Ruthu kaaya amewashukuru wanawake kwa kuwajali wazee .
Naye Meneja wa kituo hicho Moses Mafie amesema kituo hicho kinacho wahudumia wazee 300 wasiojiweza kilianzishwa kikilenga kuwasaidia wazee wasio na makazi
Bi. Julieth Maturo akikabidhi msaada kwa Wazee.
wazee wakishukutu na kuomba wadau wengine kujitokeza kuendelea kuwasaidia mahitaji muhimu.
Meneja wa kituo cha wazee Ndg. Mafie
Ummoja wa wanawake Halmashauri ya Wilaya ya meru wakiwa makazi ya wazee.
Kamati tendaji ya umoja wa wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2021.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa