Wanawake wapatao 123 Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamenufaika na ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Usa –River kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru,ikiwa ni baada ya Serikali kutoa Milioni 500 kwaajili ya ujenzi na Ukarabati wa Kituo Hicho.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Usa – River, Dkt.Hillary Mkini amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma ya Upasuaji kituoni hapo tarehe 17 Septemba 2019 jumla ya wagonjwa 132 wamefanyiwa upasuaji, kati yao kinamama wajawazito ni 123 na wagonjwa 9 walifanyiwa upasuaji wa kawaida .
Dkt.Mkini amesema kunaongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa wanahudumiwa kituoni hapo ambapo kabla ya uboreshaji idadi ya wagonjwa ilikuwa wagonjwa 600 hadi 800 kwa Mwezi na Wakiongezeka sana walifika 1,200 tofauti na sasa ambapo idadi ya wagonjwa ni 2,500 hadi 3,000 kwa mwezi.
Mkini amehitimisha kwa kutoa wito kwa jamii kupata huduma katika kituo hicho na kueleza kuwa hali za wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji kituoni hapo zilikuwa nzuri na wote waliruhusiwa kwenda Majumbani .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg. Emmanuel J. Mkongo amesema uboreshaji wa Sekta ya Afya ni kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya katika umbali mdogo.
Mkongo ameishukuru Serikali kwa kutoa Shilingi milioni 500 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Usa -River hususani ujenzi wa majengo mapya 6 ambayo ni jengo la upasuaji, nyumba ya mtumishi, jengo la maabara, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuhifadhia maiti na kichomea taka pamoja na kufanya ukarabati wa majengo 3 yaliyokuwepo ambayo ni Jengo la kuwahudumia wagonjwa wa nje (OPD), jengo la duka la dawa ambalo awali lilitumika kama kama jengo la Maabara na Jengo wodi ya wanawake na watoto.
Naye Witness Ayo ambaye ni mkazi wa Leguruki aliyeweka rekodi ya uzinduzi wa huduma ya upasuaji katika Kituo hicho tarehe 17 Septemba 2019 ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuboresha sekta ya Afya kwani imeokoa maisha ya kinamama wengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg. Emmanuel J. Mkongo.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Usa – River, Dkt.Hillary Mkini
Jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Usa – River.
Jengo la Wodi ya mama na mtoto katika kituo cha Afya Usa – River.
Jengo la maabara katika kituo cha Afya Usa – River.
Nyumba ya mtumishi katika kituo cha Afya Usa – River.
Wananchi wakipata huduma katika Jengo la kuwahudumia wagonjwa wa nje (OPD)
.
Muonekano wa ndani wa jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Usa - River.
Taa maalumu katika chumba cha upasuaji kituo cha Afya Usa river.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa