Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa vituo vya Kupiga Kura na wasaidizi wao, wa Uchaguzi mdogo wa nafasi ya diwani Kata ya Songoro utakaofanyika tarehe 12 Agosti, 2018, kusimamia vituo hivyo Kwa umakini ili wapiga kura wapige kura Kwa uhuru.
Akiongea wakati wa mafunzo elekezi Kwa wasimamizi hao yaliyo fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Leo tarehe 9 Agosti, 2018, Mkurugenzi Kazeri amefafanua kuwa ni muhimu kwa wasimamizi hao kuwa makini wakati wa mafunzo ili kupata uelewa wakutosha wa kusimamia zoezi la upigaji kura kwenye uchaguzi mdogo huo."Fuatilieni mafunzo haya Kwa umakini na hata msipoelewa vizuri kanuni na Sheria za kusimamia vituo ulizeni maswali tunataka uchaguzi uwe wa huru na haki kama Tume ya uchaguzi "amesisitiza Kazeri.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amewataka wananchi wa kata ya Songoro wenye sifa ya kupiga Kura kujitokeza kupiga kura na Kumchagua mwakilishi wao ambae atawaletea maelendeleo katika Kata yao ya Songoro.
Uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Songoro unafanyika baada ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kutangaza uchaguzi huo Kwa mujibu wa Sheria ya uchaguzi ya hapa nchini.
Ikumbukwe kuwa Kata ya Songoro ni miongoni mwa Kata 26 za Jimbo la uchaguzi la Arumeru Mashariki.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa vituo vya Kupiga Kura na wasaidizi wao
Baadhi ya wasimamizi wa vituo vya Kupiga Kura na wasaidizi wao
Baadhi ya wasimamizi wa vituo vya Kupiga Kura na wasaidizi wao
Baadhi ya wasimamizi wa vituo vya Kupiga Kura na wasaidizi wao
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa