Mkuu wa Divisheni ya Usafi na Mazingira Charles Makama amefungua Mafunzo ya Wastaafu watarajiwa Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya kupitia Mafunzo yaliyohusisha wastaafu watarajiwa takribani 71 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuratibiwa na Ofisi ya Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Lengo la Mafunzo hayo likiwa ni Kujua stahiki mbalimbali za wastaafu kabla na baada ya kustaafu, Kutatua changamoto za Michango kabla ya kustaafu, Kuwapatia Elimu ya Mafao baada ya Mafao na maisha mara baada ya kustaafu Kwa Ujumla.
Aidha washiriki wametoa Pongezi za dhati Kwa Mkurugenzi Mtendaji kwani wanakiri Jambo hili halijawai kutokea pia wameridhika na Mafunzo waliyoyapata kwani wamefunguliwa mambo mengi waliokuwa hawajui na sasa wanayafahamu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa