Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amewataka watumishi na mawakala wote wanaokusanya mapato ya Halmashauri hiyo kutumia mashine za POS kuhakikisha wanatoa risiti pindi wapokeapo malipo sambamba na kuwa na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato hayo.
Makwinya amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya timu maalum iliyofanya tathimini juu ya ukusanyaji mapato katika machinjio ya Tengeru kwa muda wa siku 12 ambapo ilibaini uwepo wa uzembe wa baadhi ya wataalam wa mifugo kutokufika kwa wakati eneo la machinjio, risiti za malipo kutokutolewa kwa wakati nk.
Mwl.Makwinya ameiagiza Idara ya Afya kuhakikisha usalama wa nyama unaendelea kuwepo kwa kufuatilia na kuhakikisha nyama zinakaguliwa kabla ya kuanza kuuzwa ,pia amewataka wataalam wa mifugo kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
Ikumbukwe kuwa tarehe 12 Agosti 2021 Mkurugenzi Zainabu alibainisha vipao mbele vyake ikiwemo kubuni vyanzo vipya vya mapato na kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa