Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Jonathan Kiama amewataka wandikishaji wa orodha ya wapiga kura kuzingatia mafunzo ya kuwajengea uwezo jinsi kuandikisha na kuandaa orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za mitaa yanayo endelea ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uchaguzi huo.
Akifungua mafunzo hayo,kiama amewataka waandikishaji hao kusikiliza mafunzo kwa umakini na kuuliza maswali ili kupata kupata uelewa wa kina kwani uandikishaji wa orodha ya mpiga kura unaumuhimu mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ni zoezi pekee linalompa haki mwananchi ya kumpigia kura kiongozi atakaye leta maendeleo.
Kiama amesisitiza baada ya mafunzo haya ni muhimu kwa wanachi wenye sifa kujiandikisha kupiga kura katika zoezi la uandikishaji orodha ya mpiga kura litakalofanyika tarehe 08 hadi 14 Octoba 2019 , kwani mwananchi ambae hatajiandikisha hatoweza kupiga kura wakati wa uchaguzi tarehe 24 Novemba 2019, kuwachagua viongozi wa Serikali za mitaa ambao ni Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji,Wajumbe wa Serikali za vijiji kundi mchanganyiko,Wajumbe wa Serikali zavijiji kundi maalumu.
Naye afisa uchaguzi kwenye Halmashauri hiyo Ndg.Edward Chitete ametoa wito kwa wandikishaji hao wa orodha ya mpiga kura pindi kutimiza wajibu wao kwa uadilifu mkubwa na kuwahudumia wananchi kwa kutumia lugha zenye staa.
Semina hiyo ya siku mbili kwa kwa waandikishaji wa orodha ya mpiga kura inaendelea katika ukumbi wa chuo cha ualimu patandi ambapo waandikishaji wa orodha ya mpiga kura wamekula kiapo cha uaminifu na kiapo cha utii na uadilifu.
Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Jonathan Kiama.
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Edward Chitete.
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Miongoni mwa wasaidizi wasaidizi ngazi ya Halmashauri Bi.Grace Mbilinyi wakati wa Semina .
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Miongoni mwa wasaidizi wasaidizi ngazi ya Halmashauri Ndg.Juma wakati wa Semina .
Baadhi ya Wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wakati wa mafunzo.
Waandikishaji wa orodha ya mpiga kura wakati wa kiapo cha uaminifu na kiapo cha utii na uadilifu.
Waandikishaji wa orodha ya mpiga kura wakati wa kiapo cha uaminifu na kiapo cha utii na uadilifu.
Waandikishaji wa orodha ya mpiga kura wakati wa kiapo cha uaminifu na kiapo cha utii na uadilifu.
Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata.
Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata.
Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata.
Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa