Watumishi wa idara ya utawala na rasilimali watu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru watakiwa kutekeleza majukumu ipasavyo kwa kutoa huduma bora na zenye tija ,watumishi hao wamekumbushwa hayo na kaimu mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Ndg.Edward Chitete wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
akizungumza wakati wa kikao hicho ndg.Chitete amewaonya watumishi hao kutojihusisha na rushwa kwani kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria pia amewataka kuacha utoro kwa kuhakikisha wanafika kwenye vituo vyao vya kazi kwa wakati akisisitiza kuwa "usifike kwenye kituo ukajioredhesha kwenye daftari la mahudhuri ukaondoka,hakikisha unakwepo kwenyekituochako cha kazi muda wote wa saa za kazi na unawajibika ipasavyo" amesema kaimu wa idara ya utawala na rasilimali watu.
Aidha elimu juu ya namna ya kutekeleza majukumu ya kila kada iliopo chini ya idara ya utawala na rasilimali watu imetolewa ambapo watumishi walio chini ya idara hiyo ambao ni watendaji wa Kata na Vijiji wamehimizwa kuiwakilisha vyema Serikali kwa wanachi wanaowahudumia kila siku kwani wanatekeleza majukumu yao kwa niaba ya Serikali hivyo watekeleze kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu ikiwa ni kwa kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi kwa wakati , kudhibiti uharibifu wa mazingira ,kushiriki katika kukusanya mapato ya Halmashauri hiyo kwa kuhakikisha wafanya biashara kwenye maeneo yao wamelipa kodi sambamba na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Mmoja wa watendaji wa kijiji (jina limehifadhiwa) amesema Chitete.
Baada ya kutoa ufafanuzi wa kisheria juu ya changamoto ya wananchi kutohudhuria mikutano Kaimu mkuu wa idara ya utumishi na rasilimali watu Ndg. Edward Chitete ametoa wito kwa wananchi kutekeleza wajibu wao ikiwa ni utoaji wa maoni yao kwenye mikutano mikuu ya vijiji hivyo wanapaswa kuhudhuria.
Idara ya Utawala na rasilimali watu inautaratibu wa kufanya vikao vyake kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kukumbushana majukumu pamoja na kutatua changamoto kwa watumishi hao kwenye kutekeleza majukumu yao.
Kaimu mkuu wa Idara ya utawala na rasilimali watu ndg.Edward Chitete akizungumza wakati wa kikao cha idara ya utawala na rasilimali
Watumishi waliopo chini ya idara ya utawala na rasilimali watu wakisikiliza mafunzo na maelekezo yanayotolewa wakati wa kikao cha idara hiyo

Afisa Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Aimbora Nnko akizungumzia umuhimu wa michezo hususani mazoezi huimarisha afya ya mwili wakati wa kikao cha idara ya utawala na rasilimali
Afisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Noel Pallangyo akizungumzia taratibu za kufanya biashara ni pamoja na kulipa kodi.
Kaimu Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Charles Mungure akizungumzia utunzaji wa mazingira kwa ujumla wakati wa kikao cha idara ya utawala na rasilimali
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa