Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi, Richard Ruyango wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja katika Benki ya NMB tawi la Usa River, amepongeza Juhudi na ubunifu wa Benki ya NMB, ya kuwa na Kiapo cha utoaji huduma kwa usikivu na weledi mkubwa ikiwa ni pamoja na kutunza taarifa za wateja, ambapo amehimiza Benki hiyo kuzingatia Kiapo ilichojiwekea Ili kiwe na tija zaidi.
Meneja wa NMB tawi la Usa-River Ndg. Mitabalulo Elisha Semuguruka akisoma taarifa ya maadhimisho ya wiki ya Mteja kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Taifa, amesema katika maadhimisho hayo Benki hiyo imezindua rasmi Kiapo cha huduma kwa wateja kikilenga utoaji wa huduma za uhakika na kuaminika, usikivu, weledi, uaminifu na kutunza taarifa za wateja kwa lengo la kutoa huduma Bora zaidi na shindanishi zenye tija kwa Benki na wateja wake.
Semeguruka amewatambua na kuwashukuru wateja wa Benki hiyo wakiwemo Watumishi wa Serikali na wasio wa Serikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo na wateja wengine wote, ambapo amewakaribisha kuendelea kunufaika na huduma nafuu na rafiki za Benki ya NMB, ambayo ameitaja kuwa benki kubwa kwani ina matawi mijini na Vijiji pia inaongoza kwa kutengeneza faida.
Vilevile ameongeza kuwa, NMB ina huduma zenye manufaa kwa wateja wake ikiwepo mikopo yenye riba nafuu na Pia Benki hiyo inatoa fursa na kumwezesha Mteja kujitengenezea faida mpaka kufikia asilimia 12% kupitia huduma ya WEKEZA AKAUNTI ambayo Mteja hulipwa faida ya asilimia 12% ya kiasi Cha fedha alichowekeza kwa kipindi Cha mwaka mmoja na malipo hufanyika Mara mbili kwa Mwaka.
Pia Mteja Anaruhusiwa kutoa asilimia 20% ya kiasi alichoweka bila masharti na Mteja anapata bima ya Maisha Mara ajiungapo na huduma hiyo ikiwa ni malipo mara mbili ya kiasi alichowekeza benki.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya amesema Halmashauri hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB katika Swala zima la maendeleo na utoaji wa huduma Bora kwa umma.
Ikumbukwe, Dunia huadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba na kwa Mwaka huu Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni *Nguvu ya Huduma*
Baadhi ya picha za tukio
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi, Richard Ruyango ,Meneja wa NMB tawi la Usa-River Ndg. Mitabalulo Elisha Semuguruka (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya, wakati wauzinduzi wa Wiki ya huduma kwa wateja tawi la NMB Usa River.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru ,Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Arumeru ,Meneja na Wafanyakazi wa NMB tawi la Usa River .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la NMB Usa River
Wafanyakazi wa NMB wakiwa katika sare maalum wakati wa maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa NMB tawi la Usa-River Ndg. Mitabalulo Elisha Semuguruka akisoma taarifa ya maadhimisho ya wiki ya Mteja .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa