Watendaji 20 wa vijiji ambao walishinda usaili uliofanyika tarehe 01 na 02 Februari 2018 wamejaza fomu za Mkataba wa Ajira Serikalini na mifuko ya hifadhi ya jamii ,hii ni baada ya kupewa semina elekezi juu ya kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma na sheria muhimu kwa uongozi wa ofisi za Kata,Serikali za Vijiji,Wenyeviti wa Vitongoji na wenyeviti wa mitaa.
Akizungumza wakati wa semina elekezi kwa watendaji hao Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu Grace A. Mbilinyi amewahimiza watendaji hao wa vijiji kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria ,Kanuni Na taratibu za Utumishi wa Umma,nukuu “mmepewa ofisi za umma kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao”
Aidha Semina hiyo imefanywa na Halmashauri ya Meru kupitia idara ya Utumishi na Rasilimali watu ikiwa ni baada ya vyeti vya watumishi hawo kuhakikiwa na Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) na kuthibitika kua ni halali
Picha za tukio.
Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu Grace A. Mbilinyi akizungumza na watendaji wa Vijiji.
Mmoja wa Watendaji wa Vijiji waliajiriwa ndg. Onesmo D. Pallangyo akiuliza swali ili kupata uelewa zaidi
Watendaji wa Vijiji walioajiriwa wakifuatilia kwa makini semina elekezi.
Watendaji wa Vijiji walioajiriwa wakifuatilia kwa makini semina elekezi.
Watendaji wa Vijiji walioajiriwa wakifuatilia kwa makini wakati wa semina elekezi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa