Mhasibu wa Halmashauri Neema Munisi ametoa elimu kwa Watendaji wa Kata na Vijiji kufuatilia leseni za biashara kwenye maeneo yao pamoja na kufanya masawazisho ya Fedha za Miradi ya maendeleo zinazopelekwa kwenye akaunti za vijiji.
Pia, amewasisitiza Watendaji kusimamia suala la ukusanyaji wa mapato kwani mapato mengi yanapatikana katika Kata na Vijiji vyao.
Aidha,amewataka watendaji wa Vijiji na Kata kuzisimamia Mashine za Ukusanyaji wa Mapato (POSS MACHINE) zilizopo Vijijini pindi zinapokusanya Fedha na kupeleka Fedha hizo benki kwa wakati .
Ametoa maelezo hayo kwenye kikao kazi cha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Watendaji wa Kata na Vijiji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa