Watendaji wa Kata Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru wameingia mkataba wa upangaji,ufuatiliaji na utekelezaji wa afua za lishe ili kufanikisha swala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika jamii ikiwemo udumavu.
Mkataba huo walio saini baina yao na Mwa jiri (Mkurugenzi ) unatoa wajibu kwa Kata kuhakikisha Lishe ni Ajenda ya kudumu pia utachochezi na kuibua fursa za lishe kwa kutatua matatizo ya lishe .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo , Ngd.Emmanue Mkongo amewataka Waten daji hao kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa mkataba huo kwani Serikali imeandaa Mikataba hiyo, kuanzia ngazi za Mikoa hadi kwenye jamii kufanikisha suala la kuboresh a hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika Kata na Vijiji.
Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Bi.Asia Ijumaa amesema hali ya utapiamlo bado ni changamoto hapa Nchini ambapo imefikia asilimia 34% hivyo jamii inapaswa kuzingatia Lishe.
Aidha Bi.Asia amesema utapiamlo unasababishwa na ulishaji duni,magonjwa ya mara kwa mara na huduma hafifu ya malezi na makuzi ya awali ya watoto wadogo , hivyo ametoa rai kwa jamii kuwasaidia kinamama kunyonyesha maziwa yao pekee miezi sita ya mwanzo pia kuendelea kunyonyesha hadi miaka miwili.
Asia amesema jamii inapaswa kulipa kipaumbele swala la lishe kwani utapiamlo husababisha vifo,kuchelewa kukua kwa vijngo na akili ya mtoto .
Maafisa Watendaji hao wamesema watahakikisha wanaifanyia kazi rasimu ya mkataba hiyo na kuisimamia lwenye vijiji vilivyopo kwenye kata zao"tutafanya Kikao cha Kata ambapo wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji watahudhuria ili kuelimishana juu ya lishe na kuweka mipango ya kuhakikisha jamii inazingatia swala la lishe" ameeleza Christina Kessy Mtendaji wa Kata ya Shambarai Burka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Ndg.Emmanue Mkongo.
Mkurugenzi Mkongo na Afisa Lishe, Asia Ijumaa.
Mkuu wa Idaraya Utawala na Rasilimali Watu,Grace Mbilinyi,ambaye Watendaji wapo kwenye idara hiyo.
watendaji wa Kata wakati wa Kikao cha kutia Saini Mkataba.

Mtendaji wa Kata ya Shambarai Burka Bi.Christina Kessy .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa