Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amewata Watendaji wa Kata wa Halmashauri hiyo kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuiwakilisha vyema Serikali ikiwa ni pamoja na kushirikina na Waheshimiwa Madiwani katika kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kuwasilisha kwa wakati taarifa za shughuli zote zinazotekelezwa kwenye Kata ikiwemo miradi ya wafadhili.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa baraza la Madiwa Mwl.Makwinya amesema ni muhimu kwa watendaji hao kuwasilisha taarifa za miradi ya wafadhili kabla ya kuanza kutekelezwa ili kuleta tija na ufanisi zaidi pamoja na kuwashirikisha Madiwani ambao ndio wenyeviti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata, shughuli zote za maendeleo zinazotekelezwa ndani ya Kata.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili ametoa wito kwa Madiwani kufuatilia shughuli mbalimbali zinazotekelezwa ndani ya Kata ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kuwaletea wananchi maendeleo" tunamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi katika sekta ya afya,elimu ,maji ,barabara hakika Meru tumenufaika "amesema Mhe.Kishili
Mhe. Dauson Urio Diwani wa Kata ya Uwiro amesema Kata nyingi zinafanya vizuri kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Diwani na Mtendaji wa Kata ambapo amesema endapo ushirikiano usipokuwepo unaathiri uhamasishaji wa wananchi kwenye shughuli za maendeleo
Naye Mhe.Glory Kaaya Diwani viti maalum Kata ya Kata ya Kikwe amesema utoaji wa taarifa wa miradi inayotekelezwa kwenye Kata ni muhimu sana kwani itasaidia Wananchi kuijuia na kishirikikatika utekelezaji wa miradi hiyo .
Aidha ,Baraza hilo la Madiwani limekamilikwa kwa siku ya kwanza mbapo madiwani wamewasilisha taarifa za utekelezaji za Kata zote 26 na utaendelea kwa siku ya pili tarehe 08 Septemba 2022
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa