Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amewataka Watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kutatua changamoto na kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika halmashauri hiyo ikiwa ni kutoa huduma rafiki kwa wananchi.
Mhandisi Ruyango ameagiza hayo wakati akikabidhi Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha mapinduzi CCM kwa
Watendaji wa Kata 26 za Halmashauri hiyo ambapo amewahimiza kuwa na mpango kazi unaolenga utekelezaji wa Ilani ya CCM katika maeneo yao "sisi kama Serikali tunasimamia na Kutekeleza ilani hii iliyopewa ridhaa na wananchi, niwatake mkasome na Kutekeleza ilani hii inayolenga utoaji wa huduma Bora kwa wananchi sambamba na kuwaletea maendeleo" amehimiza Ruyango
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amesema Halmashauri hiyo imenunua na kugawa ilani kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watendaji wa Kata Ili kuwawezesha Kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwani kwa mujibu wa katiba ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndio inayoiongoza Serikali na Chama hicho ndicho kinacho simamia Serikali" Hamna namna utafanya Kazi nje ya utekelezaji wa Ilani ya CCM hivyo ilani ni nyenzo muhimu izingatieni" amehimiza Mwl. Makwinya
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili ametoa wito kwa Watendaji na Madiwani kuwa wamoja katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwani Umoja ni msingi wa utendaji bora
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Watendaji hao wamemshukuru Halmashauri kuwanunulia nyenzo hiyo muhimu na kuahidi kusoma na Kutekeleza ilani hiyo Ili kuharakisha Maendeleo sambamba na utoaji wa huduma Bora kwa Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na Watendaji wa Kata .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Akikabidhi Ilani ya CCM kwa Eline Mamuya Mtendaji wa Kata ya Nkoaranga.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru pamoja na Watendaji wa Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa