Watendaji wa Kata kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamepewa semina kuwajengea uwezo ili kuzingatia mabadiliko ya tabia ya nchi katika uandaaji wa mipango ya maendeleo jambo litakalo punguza athari zitokanazo na maafa mbalimbali yanayo sababishwa na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ndg. Edmund Mabhuye toka Chuo kikuu cha Dar es salaam kituo cha stadi za mabadiliko ya tabia ya nchi ambaye pia ni mshauri wa mradi wa mfumo wa utoaji wa tahadhari ulio chini ya ofisi ya Waziri mkuu ameeleza kuwa kuna umuhimu wa jamii kupata uwelewa wa kina juu ya mabadiliko ya tabiaa ya nchi kwani itawawezesha kujiandaa na kukabiliana na madhara ya majanga mbalimbali yatokanayo na mabadaliko ya tabia ya nchi . Nukuu"tutumie mabadiliko ya tabia ya Nchi kama fursa" amesema Mabuye.
Mtendaji wa Kata ya Majengo ndg. Yohana S. Mollel ameishukuru Serikali kwa juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha juu ya athari za majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya Nchi na kuweza kujiandaa pamoja na kukabiliana nayo kwa kuwajengea uwezo kupitia mafunzo mbali mbali yanayotolewa kwa wananchii hao na viongoji kuanzia ngazi za chini .
Yohana amesema Kata ya Majengo ni miongoni mwa kata zinazoathirika na janga la mafuriko mara kwa mara yanayosababisha maafa kama vile uharibifu wa makazi ya wananchi pamoja na miundombini ya barabara hivyo atatumia mafunzo hayo kuelimisha kamati ya maafa kwenye Kata yake kuzingatia mabadiliko ya tabiaa ya nchi kwenye mipango ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2018/2019 pia amebainisha kutokana na mafunzo mbalimbali yaliyotolewa wananchi wameweza kutumia taarifa za haliya hewa wanazopokea kupitia simu zao za mikononi na kuzitumia "mwezi Februari 2018 wananchi wa kata hiyo walipata taarifa za kuwepo kwa mvua nyingi mwanzoni mwa mwezi Machi 2018 hivyo tume hamasisha wananchi walio kwenye maeneo yanayokubwa na mafuriko kuhama" amesema Yohana.
Mratibu wa maafa kwenye Halmashauri hiyo Digna Masawe amesema kamati ya maafa wilaya imejipanga vyema kuhakikisha kila kata na Vijiji zimeunda kamati za maafa na zinafanya kazi na kuleta tija kwenye jamii.
Naye kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga amewataka watendaji hao wa Kata na wataalamu kutumia mafunzo hayo muhimu katika kutekeleza majukumu yaho.
Picha za tukio.
Ndg. Edmund Mabhuye toka Chuo kikuu cha Dar es salaam kituo cha stadi za mabadiliko ya tabia ya nchi ambaye pia ni mshauri wa mradi wa mfumo wa utoaji wa tahadhari ulio chini ya ofisi ya waziri mkuu akitoa mafunzo kwa watendaji wa Kata juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Miongoni mwa Watendajin wa Kata wakifuatila mafunzo ya mabadiliko ya tabia ya Nchi yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Miongoni mwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatila mafunzo ya mabadiliko ya tabia ya Nchi yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Amani Sanga akizungumza wakati wa kuhairisha semina ya mabadiliko ya tabia ya Nchi ,kulia kwake ni Mratibu wa maafa kwenye Halmashauri hiyo ndg. Digna Masawe na kushoto kwake ni Ndg. Edmund Mabhuye toka Chuo kikuu cha Dar es salaam kituo cha stadi za mabadiliko ya tabia ya nchi .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa