Watendaji wa Vijiji na Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru watakiwa kutekeleza wajibu wao kisheria kwa kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa waliopo mashuleni wanahudhuria na kumaliza elimu ya msingi.
Hayo yameelezwa na Afisa elimu vifaa na Takwimu wa halmashauri hiyoTheodosia Haule kwenye kikao kazi cha Walimu wakuu na watendaji wa Kata na vijiji kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mariado, kikiwa na lengo la kukumbushana majukumu kwa kuzingatia Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ili kuboresha elimu, Pia amewasihi walimu wakuu kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa Kata na Vijiji jambo litakalo rahisisha kudhibiti ajira za utotoni,mimba kwa wanafunzi pamoja na utoro kwa wanafunzi na walimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa