Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Emmanuel Mkongo amewataka watendaji wa Kata na Vijiji kuendana na malengo ya Serikali ya awamu ya tano kwa kukusanya mapato ipasavyo yatakayo waletea wananchi maendeleo.
Mkurugenzi Mkongo ameeleza hayo wakati wa kikao cha Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu, ambapo amewataka watendaji hao kusimamia suala zima la ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika maeneo yao pamoja na kuzingatia Sheria ,Kanuni na taratibu kwenye matumizi ya fedha na manunuzi.
Mkurugenzi Mkongo amewasisitiza watendaji hao kusimamia utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao ,sambamba na kuhamasishwa wananchi kutambua wajibu wao wa kushiriki katika utekelezaji na utunzaji wa miradi hiyo.
Mkurugenzi Mkongo ameongeza kuwa uwazi na uwajibikaji ni swala muhimu kwenye kutekeleza majukumu , hivyo amewataka watendaji hao kufanya mikutano yote kwa wakati na kubandika taarifa za mapokezi ya fedha na zile za matumizi kwenye mbao za matangazo, “itisheni mikutano mikuu ya Vijiji muwasomee wananchi taarifa za mapato na matumizi kwa wakati kuepuka sintofahamu” amesisitiza Mkongo.
Mkurugenzi Mkongo amehitimisha kwa kuwataka watumishi wote wa idara hiyo ya Utawala na rasilimaliwatu kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu.
Naye Abel Kaaya ambae nia Mtendaji wa Kata ya Ambureni akizungumza kwa niaba ya Watumishi wenzake , amempongeza Mkurugenzi Mkongo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya Ukurugenzi na kumwahidi kumpa ushirikiano wa kutosha .
Hayo yamejiri katika Kikao hicho cha kawaida cha kila wa mwezi cha Idara ya Utawala na rasilimali watu katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya mwezi.
PICHA ZA TUKIO.
Mkurugenzi Emmanuel Mkongo akizungumza na Watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu.
Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Grace Mbilinyi akitoa ufafanuzi wa kikao cha idara yake ambocho hufanyika kila mwezi.
Maafisa Utumishi wakimsikiliza Mkurugenzi wakati wa kikao.
Watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji.

Mtendaji wa Kata ya Ambureni Abeli Kaaya akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa