Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher J. Kazeri amewataka watendaji wa vijiji kwenye Halmashauri hiyo kutoa huduma bora kwa wananchi kwani baadhi ya watendaji hao wanalalamikiwa na wananchi.
Mkurugenzi Kazeri ameeleza hayo kwenye kikao cha idara ya utawala na Rasilimali watu kilichofanyikia katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo alitia msisitizo kwa watendaji hao kuiwakilisha vyema Serikali kwa kutoa huduma bora akitumia mfano " nyie ni wakurugenzi wa vijiji" , pia amewakumbusha kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusaidia swala zima la ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuhakikisha wafanyabiashara wote kwenye maeneo yao wana leseni za biashara na kudhibiti uharibifu wa mazingira.
Mmoja wa watendeji hao Sakina A.Safari ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Kolila kata ya Malula amesema wapo tayari kutekeleza majukumu yao likiwemo kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa