• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU WATAKIWA KUTEKELEZA WAJIBU WAO KUENDANA NA KASI YA AWAMU YA TANO.

Imewekwa: February 27th, 2020

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Ndg.Richard Kwitega amewataka Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru, mkoani humo kutekeleza wajibu wao kuendana na kasi ya awamu ya tano iliyojikita kwenye utawala bora na kuwaletea wananchi maendeleo .

Kwitega amesema hayo Wakati wa Ziara yake katika Halmashauri hiyo inayolenga kukumbusha wajibu na utendaji ,kuona changamoto zinazowakabili Watumishi na namna ya kuzitatua, ambapo amesema watumishi hao hawana budi kutimiza majukumu yao kwa weledi na ufanisi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora ili kuwaletea maendeleo wananchi "kila Mtumishi wa umma ana umuhimu kwa nafasi aliyonayo katika swala la maendeleo " amesema Kwitega

Kwitega ametoa wito kwa Watumishi hao kuwa na maadili ndani na nje ya vituo vyao vya kazi ikiwa ni kuepuka rushwa ,ulevi wa kupindukia pia amekemea kitendo cha baadhi ya watumishi kukopa mitaani kwa dhamana ya kadi zao za benki badala yake wakope kwenye taasisi za fedha kwa utaratibu wa kukopesha Watumishi wa Umma uliowekwa na Serikali "kopeni kwa utaratibu kuepuka kudhalilisha Utumishi wa Umma" amesisitiza Kwitega

Aidha Ndg.Kwitega amewapongeza Watumishi wa Wilaya ya Arumeru kwa utendaji wao unatia fora na kuwezesha Wilaya hiyo kufanya vizuri kwenye Sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu ambapo katika matokeo kidato cha sita mwaka 2019 Shule zake mbili zilifanya vizuri ambapo Shule  ya Sekondari Kisimiri ilishika nafasi ya kwanza kitaifa na Shule ya Sekondari Mwandeti ilishika nafasi ya Nne..

Akihitimisha  Kwitega amewataka watumishi hao kujitathimini kwa nafasi walizo nazo ni kwa namna gani wametekeleza wajibu wao ili kuwaletea maendeleo.

Awali Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimaliwatu. Ndg. David Lyamongi amesema Utumishi wa Umma unaongozwa kwa Sheria na Taratibu ambapo aliweka bayana utaratibu wa stahiki za watumishi wa Umma ikiwa ni upandaji wa madaraja na ubadilishaji vyeo, uhamisho, posho mbalimbali katika utumishi wa Umma , utaratibu wa likizo na ushughulikiaji na ulipaji wa madeni ya watumishi.Ambapo ametoa wito kwa Viongozi na Watumishi kuzingatia Sheria na Taratibu hizo.

Naye katibu tawala wa Wilaya ya Arumeru Mwl. James Nchembe amemshukuru Katibu Tawala Mkoa wa Arusha kwa kupongeza utendaji wa Wilaya hiyo yenye watu zaidi ya laki saba na kuahidi kuendelea kufanya kazi kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.

ziara ya Katibu tawala Mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Arumeru imekamilika katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo Katibu Tawala amezungumza na  watumishi wa tarafa za Poli, Mbuguni na King’ori na itaendeleo siku ya Pili katika Halmashauri ya Arusha.

Baadhi ya watumishi waliopata fursa ya kutoa maoni wamepongeza kitendo cha Katibu Tawala Mkoa wa Arusha kufanya ziara hiyo ya kuwakumbusha wajibu wao sambamba na kupokea changamoto walizonazo na kuzitatua na kuomba vikao kama hivyo kuwa endelevu kuanzia ngazi ya Halmashauri "tunaomba vikao vya namna hii kuendelea kuwepo kwa ngazi mbalimbali kwani vitaleta tija kwenye utendaji wetu " alisihi Ndg. Erick Kulindwa ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Kingori .

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Ndg.Richard Kwitaga akizungumza na Watumishi wa Tarafa ya Poli na Mbuguni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimaliwatu. Ndg. David Lyamongi akizungumza wakati wa Mkutano  wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha na watumishi wa Tarafa ya Poli  na Mbuguni .

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Mwl.James Nchembe akizungumza wakati wa Mkutano  wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha na watumishi wa Tarafa ya Poli  na Mbuguni .

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Dkt.Amani Sanga  akizungumza wakati wa Mkutano  wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha na watumishi wa Tarafa ya Poli  na Mbuguni .

Katibu tawala Mkoa wa Arusha Ndg.Richard Kwitaga akizungumza na Watumishi wa Tarafa ya Poli na Mbuguni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Wakuu wa idara,wa Mkutano  wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha na watumishi wa Tarafa ya Poli  Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Baadhi ya watumishi wa Tarafa ya Poli na Mbuguni wakati wa mkutano wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha katika  ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Mkutano  wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha na watumishi wa Tarafa ya Poli  Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Ndg.Richard Kwitaga akizungumza na Watumishi wa Tarafa King'ori katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru .

Katibu tawala Msaidizi David Lyamongi akizungumza wakati wa Mkutano  wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha na watumishi wa Tarafa ya King'ori.

Watumishi wa Tarafa ya King'ori wakati wa mkutano wa Katibu tawala Mkoa wa Arusha katika  Tarafa hiyo.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa