Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta amewasimamisha kazi Mtendaji Kijiji na Kata ya Mwandeti,na Afisa Tarafa ya Mukrati kuwa chini ya ungalizi ili kupisha uchuguzi zaidi na hatua kali zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.
Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao kazi kati ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Meru, Maafisa Tarafa , Watendaji wa Kata 36 na vijiji 90 pamoja na wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Aidha Mheshimiwa Kimanta amesema kuna uzembe mkubwa umefanyika katika utendaji wa majukumu yao, hasa kushindwa kudhibiti kilimo cha bangi katika maeneo yao.
“Haingii akilini tokea bangi inalimwa kwa miezi 3 na mwezi wa 4 inavunwa wewe mtendaji wa kata na kijiji upo hapo na hauchukui hatua yoyote”.
Amesema haieleweki kwanini nyie kama viongozi mmeshindwa kudhibiti kilimo cha bangi kwa muda wote huo na mpo hapohapo.
Amewataka watumishi kuacha kufanyakazi kwa mazoea kwani zama hizi niza kuwajibika kila mtu kwenye nafasi yake.
Kimanta amesisitiza zaidi kwa viongozi wa kata na vijiji kuwafichua wote wanaolima bangi katika maeneo yao badala ya kuwaficha,amesema kwa kufanya hivyo wanachangia kuiharibu jamii.
Amewataka viongozi hao wa kata na vijiji kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hivyo watakuwa wamewatumika vyema wananchi wao.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Arumeru Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Jerry Muro, amesema tatizo kubwa kwa watumishi wa wilaya hiyo ni kufanya kazi kwa mazoea ndio maana wanashindwa kuchukua hatua mbalimbali za kiutendaji katika maeneo yao.
Aidha, Muro amewataka watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wawe wabunifu zaidi katika kutekeleza majukumu yao badala ya kuwasubiria viongozi wa ngazi ya juu tu.
Mheshimiwa Kimanta amefanya ziara fupi katika wilaya ya Arumeru, baada ya maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli dhidi ya tuhuma za ulimaji bangi katika wilaya hiyo.
Watumishi 3 waliosimamishwa kazi ni wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta akizungumza wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Wakurugenzi wa Halmashauri 2 za Wilaya hiyo na Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata 26 na Vijiji 90 pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilay ya Meru.
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg. Jerry Muro amewataka watumishi wa Wilaya hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Wakuu wa Idara/Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Emmy Mfuru amesema baada ya shule kufunguliwa Walimu wameweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wanafundishwa sambamba na mihula ya masomo.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Mwl. Marcus Nazi amesema Halmashauri hiyo tarehe 4 Julai 2020 iliwapongeza Walimu na Wanafunzi Walioinua Taaluma ambapo Halmashauri hiyo ilifanya vizurii katika mtihani wa Kuhitimu Darasa la saba mwaka 2018 kutoka nafasi ya 40 hadi nafasi ya 23 mwana 2019.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa