Kaimu mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Idd Kimanta amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhakikisha lengo la Serikali la kutokomeza saratani ya shingo la mlango wa kizazi kwa kutoa chanjo kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 14 linakuwa na mafanikio makubwa.
Mhe. Idd Kimanta amesema hayo alipokua akizungumza kwenye kikao cha dharura cha watumishi kutoka idara mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwemo wakuu wa idara na vitengo,watendaji wa kata na vijiji,waratibu wa elimu wa kata,maafisa maendeleo ya jamii wa vijiji na kata pamoja na watumishi wasio wakuu wa idara na vitengo wa makao makuu ya Halmashauri hiyo ambapo alieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano baada ya kuingia madarakani ikiwa na lengo la kuboresha sekta mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora imeboresha sekta ya Afya kwa kuongeza bajeti yake kutoka bilioni 34 hadi bilioni 269 .
Mhe.Idd Kimanta mbali na kuzungumzia masuala ya chanjo ya kinga ya saratani ya shingo la kizazi (HPV) amewatakia watumishi hao maadhimisho mema ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwasihi kuadhimisha kwa amani, pia amewakumbusha kutambua kuwa wameajiriwa na serikali ili kuiwakilisha vyema hivyo watumie taaluma zao na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu huku akiwaonya kutojihusisha na siasa ,"kazi za siasa waachie wanasiasa"amesisitiza Mhe. Kimanta.
Mhe Kimaths amehitimisha mazungumzo kwa kuwapongeza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwani kwa muda mfupi ameridhishwa na uchapakazi wao pia amewasihi kushiriki kikamilifu kwa kuhamasisha na kutoa elimuu juu ya janjo ya Kinga ya Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi ili Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kwenye utoaji wa Chanjo hiyo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Christopher J. Kazeri amesema amepokea ushauri wa Kaimu mkuu wa Wilaya ya Arumeru kama agizo hivyo Halmashauri itaufanyia kazi.
PICHA ZA TUKIO.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Idd Kimanta akizungumza wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Christopher J. Kazeri akizungumza wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru.
Baadhi ya wakuu wa idara/vitengo wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru.
Baadhi ya wakuu wa idara/vitengo wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru
Baadhi ya wakuu wa idara/vitengo wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Wilaya ya Meru akifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru
Baadhi ya watumishi kutoka wa idara/vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru
Baadhi ya watumishi kutoka wa idara/vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru.
Watumishi kutoka wa idara/vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru.
Baadhi ya watumishi kutoka wa idara/vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yanaendelea wakati wa wakati wa kikao cha dharura cha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa