Mafunzo ya mpango kuwezesha jamii kujiwekea akiba kwa wawezaji TASAF ngazi ya wilaya na Kata katika Halmashauri ya Meru yamekamilika kwa siku ya pili ambapo wamejengewa uwezo juu ya dhana ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu katika maswala ya uchukuaji mikopo na uendeshaji wa biashara.
Mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku 5 katika kumbi za Halmashauri hiyo yanalenga kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba kwa kaya maskini ili kuziwezesha kukabiliana na dharura na mahitaji ya msingi. Ndg.Hamnza Selemani ambaye ni mwezeshaji ngazi yaTaifa amesisitiza kuwa akiba ni chachu ya kuleta maendeleo kwenye Kaya hivyo ni muhimu Kaya husika kuwa na nidhamu ya kujitolea na kujiwekea akiba kwa malengo ya badae,.
Aidha katika swala la kutunza kumbukumbu mafunzo kwa vitendo yamefanyika kwa wawezeshaji hao kujaza daftari la kumbukumbu za wanachama, mahudhurio na fomu za mikataba ya mikopo .
Mtaalamu wa Mafunzo na Ushirikishwaji kutoka TASAF Makao makuu,Ndg.Mercy Mandawa akizungumza na wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya na Kata katika Halmashauri ya Meru.
Wawezeshaji wa wa TASAF ngazi ya Wilaya na Kata wakifanya mafunzo kwa vitendo katika vikundi.
Ndg.Hosea Mwankusye ambaye ni Kiongozi wa timu ya wawezeshaji kitaifa akisistiza jambo wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Wilaya na Kata Halmashauri ya Meru.
Wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Taifa,Ndg. Hamza Seleman na Abdallah Dokodoko(kulia) wakifafanua maswala mbalimbali wakati wa mafunzo kwa vitendo.
Hamza Seleman mwezeshaji ngazi ya Taifa akitoa mafuzo kwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya na Kata Halmashauri ya Meru..
Mwezeshaji wa wa TASAF ngazi ya Kata akiwasilisha kazi ya kundi baada ya kufanya mafunzo kwa vitendoi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa