Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo amekabidhi tena, fomu za Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki wateule wawili , Hamis J. Kiemi kupitia Chama cha CUF na Francis Silas Ringo kupitia Chama cha ADA _TADEA.
Wagombea wote wawili walifika kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi kwa nyakati tofauti na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, alimkabidhi fomu ya uteuzi wa nafasi ya Ubunge Hamis J. Kiemi kupitia Chama cha The CUF mnamo saa 6.10 mchana. Pia Francis S. Ringo wa Chama (ADA _TADEA) alikabidhiwa fomu hiyo majira ya saa 6:04 mchana .
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amewakabidhi fomu ya Uteuzi wagombea hao, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.kwenye fomu ya Uteuzi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge kwa Francis S. Ringo wa Chama (ADA _TADEA).
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge kwa Hamis J. Kiemi kupitia Chama cha CUF.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa