Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewaagiza waganga wakuu kwenye Halmashauri mbili za Wilaya Hiyo kuhakikisha kila kituo cha Afya na Hospital za Wilaya zina dirisha maalumu kwaajili ya kuwahudumia wazee.
Muro ametoa agizo hilo katika uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilayani humo na kueeleza kuwa wazee wanatakiwa kupewa huduma za afya bila kero .
Aidha agizo la Mhe.Muro ni sambamba na utengenezaji wa vitambulisho vya wazee watakavyo vitumia kupata huduma za Afya bila malipo.
Akipokea maagizo hayo Mganga Mkuu Halmashauri ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara ameeleza kuwa asilimia 80% ya wazee wanaokidhi vigezo vya msamaha wa kuchangia huduma za Afya kwa mujibu wa sera ya Afya ya mwaka 2007 wametengenezewa vitambulisho.
Dkt.Kilasara ameongeza kuwa zoezi la kuwatambua wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 ambao hawana uwezo wa kipato huanzia ngazi ya vitongoji,vijiji na Kata hivyo ametoa rai kwa viongozi wa ngazi husika kufanya utambuzi wa wazee kwa wakati ili watengenezewe vitambulisho vya matibabu bila malipo.
Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru limeshirki uboreshaji wa huduma za Afya kwa kutoa shuka 30 zitakazo tumika katika kituo cha Afya Usa-River.
Uzinduzi wa jukwaa hilo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
(kushoto) kwa mkuu wa wilaya Arumeru ni Mwenyekiti wa Jukwaa la ushirika Mkoa wa Arusha Ndg. Wilibald Ngambeki na kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wilaya ya Arumeru Mch.Anaeli Nassari.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirika Halmashauri ya Meru Mkumbwa Mussa (kulia ) pembeni yake ni Afisa ushirika kwenye Halmashauri ya Meru Neema Mundo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa