Waziri wa Nchi OR -TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo mbali na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo kwenye kituo cha afya cha Usa-river ameagiza ujenzi huo kukamilika kwa wakati ili wananchi kupata huduma bora za afya .
Mhe. Jafo amesema hayo alipokua akikagua ujenzi na uboreshaji wa kituo hicho ambacho ni miongoni mwa vituo vya Afya 200 vilivyopokea fedha toka Serikali kuu kiasi cha sh.milioni 500 kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu.
Nao wananchi wa kata ya Usa-river wameishukuru Serikali kwa uboreshaji wa kituo hicho. "kinamama tutaweza kujifungua salama kwani hapa ni karibu "amesema Sara Akyoo ambaye ni mkazi wa Kata ya Usa-river.
Aidha ujenzi unaoendelea kwenye kituo hicho cha Afya umefikia hatua za ukamilisha (finishing) kwa jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto na chumba cha kuifadhia maiti.Pia kichomea taka kimekamilika.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa