Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amezitaka Halmashauri za Meru na Arusha Wilayani Arumeru kuwabadilishia miundo watumishi sambamba na kutenga bajeti za kuwaendeleza watumishi waliopo ili kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi .
Waziri Mhagama amesema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri za Meru na Arusha Wilayani Arumeru, ambapo amebainisha ubunifu ni muhimu katika kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi waliopo.
Vilevile Mhe.Mhagama amehimiza haki za watumishi kupewa kipaumbele sambamba na kuwa na usawa kwa watumishi katika fursa na uwezeshaji toka Serikalini ili watumishi wajisikie na kujivunia kuwa sehemu katika kujenga nchi hii "niwatake Wakurugenzi kuhakikisha watumishi wa kada zote wananufaika na fursa za Serikali ya awamu ya sita pamoja na kuhakikisha watumishi wanapewa haki zao na kutatuliwa changamoto walizo nazo kwa wakati"amehimiza Mhe.Waziri Mhagama.
Mhe.Mhagama amesema Serikali imewekeza sana kwa watumishi wa umma, ambapo ametoa wito kwa Watumishi kuweka malengo na kuyatekeleza ambapo amehimiza haki kuenda sambamba na wajibu.
Pia. Mhe.Waziri Mhagama amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya kwa ujazaji wa taatifa za watumishi kwenye mifumo ambapo Halmashauri hiyo imefika zaidi ya asilimia 96%.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe .John Mongela amesema mafanikio katika sekta mbalimbali za Mkoa wa Arusha ni pamoja na mchango wa watumishi, ambapo ameahidi Mkoa kutekeleza maagizo na ma maelekezo yote ya Mhe.Waziri
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akiwasilisha taarifa ya Watumishi amesema serikali imeendelea kuboresha maslai ya watumishi katika halmashauri hiyo ambapo kwa kipindi cha mwaka mmoja imetoa mkopo usio na riba kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kiasi cha Shilingi milioni 600 kuwawezesha kununua vyombo vya usafiri, sambamba na kutoa ajira kwa watumishi 133 wa kada mbali mbali,kupandisha madaraja watumishi 1,245 ambapo amebainisha bado kunaupungufu wa watumishi 696 wa sekta mbali mbali.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha maslai ya watumishi wa kada mbali mbali hivyo kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.
Aidha,Baada ya Kuzungumza na Watumishi Mhe.Waziri anaendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo atatembelea masjala za ardhi katika Kijiji cha Maweni na Karangai.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Meru na Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe .John Mongela akizungumza wakati wa Ziara
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akiwasilisha taarifa ya Watumishi
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa ziara ya Mhe.Waziri Mhagama
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa ziara ya Mhe.Waziri Mhagama
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa ziara ya Mhe.Waziri Mhagama
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa