Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Meru (Tengeru) ikiwa ni ziara ya kupata uzoefu wa uendeshaji wa hospitali na utoaji wa huduma za afya ambapo amepata fursa ya kutembelea jengo la kitengo cha dharura (EMD) ambalo Serikali ya awamu ya sita ilitoa milioni 300 fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Aidha, Mhe. Mazrui amesema mlipuko wa UVIKO 19 umekuwa funzo kwa kila Nchi kuboresha sekta za afya kwani haikuwezekana kutegemea nchi za nje kutibu wagonjwa, hivyo katika kuboresha huduma za afya Watanzania hawana budi kushiriki maendeleo kwani fedha za wafadhili zinazoletwa zinatokana na kodi wanazolipa wananchi wa nchi hizo za wafadhili " ugonjwa hausubiri, leo hii tunaona kupitia tozo za miamala ya simu tumejenga miundombinu mbalimbali" amepongeza Mhe.Mazrui
Vilevile Mhe.Waziri Mazrui amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaimarishwa kwa vitendo na ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali ambapo amesema kunamwingiliano Mkubwa kati ya Mkoa wa Arusha na Zanzibar ambapo watalii wengi hutoka Arusha kwenda Zanzibar na Zanzibar kuja Arusha.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela amesema Serikali ya awamu ya sita inatekeleza kwa haraka utoaji wa huduma bora kwa wananchi wake ambapo kwa mwaka mmoja imetoa bilioni 3.5 fedha za tozo kwa ajili ya ujenzi wa miundombini katika sekta ya afya,elimu pamoja na ununuzi wa vifaa tiba hivyo ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana kwenye gurudumu la maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango kwa niaba ya Wananchi wa wilaya hiyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha za maendeleo ikiwa ni pamoja na fedha za tozo ambapo kwa Halmashauri hiyo Serikali katika sekta ya afya ilitoa Milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la kitengo cha dharura EMD , Shilingi Milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mareu , Shilingi Milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi Zahanati ya Maji ya chai.
Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akisaini kitabu cha wageni alipowasili Hospitali ya Wilaya ya Meru.
Waziri wa Afya Serikali ya Zanzibar akipata maelezo toka kwa mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Meru Dkt.Agness Kanusya
Picha ya Pamoja ya Mhe. Waziri Nassor Ahmed Mazrui na Viongozi mbalimbali
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa