• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

WAZIRI WA MAJI AZINDUA UREJESHAJI MTO NDURUMA KWENYE MKONDO WAKE ,ZAIDI YA MAKAZI 730 KUOKOLEWA

Imewekwa: August 26th, 2022

Arumeru,Meru

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (Mbunge) amezindua rasmi mradi wa urejeshaji Mto Nduruma kwenye mkondo wake ili kunusuru makazi 730  yaliyokuwa yakiathiriwa na mafuriko  katika Kata za Shambarai Burka  na Mbuguni, pamoja na hekari 3,280 za mashamba  na barabara 5 zenye jumla ya urefu wa Km 18.


Akizungumza baada ya uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Shambarai burka Mhe.Waziri Aweso amesema  Serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan inahakikisha wananchi wake wapo salama kwani imetoa milioni 250 za mradi huo wa kurejesha Mto kwenye mkondo wake ili kudhibiti mafuriko "Serikali ilisikia kilio chenu na kuleta fedha hizi, nitoe wito kwenu kutokufanya shughuli au kuharibu vyanzo vya maji kwani  jukumu la kutunza vyanzo vya maji ni jukumu letu sote " amehimiza Mhe. Aweso


Mhe. Aweso amesema wananchi na viongozi hawana budi kutunza vyanzo vya Maji  kwani maji hayana mbadala na kwakuwa ni uai hakuna uai bila maji ambapo amewaagiza Wakurugenzi wa Mabonde yote ya maji nchini likiwemo bonde la pangani  kutembelea na kuvitambua vyanzo vya maji kwa kuweka mipaka sambamba na kushirikiana na Maafisa wa mazingira wa halmashauri katika shughuli za mazingira "haipendezi mnaacha watu  kupanda mazao kwenye vyanzo vya maji hadi  yanakomaa ndio mnayaharibu kwani wakati wanaanza kupanda mlikuwa wapi? " amehoji Mhe.Aweso


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe.Dkt.John D. Pallangyo amesema Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwaletea maendeleo Wananchi wa Arumeru kwani changamoto ya mafuriko ilikuwa kikwazo kikubwa hivyo anaishukuru Serikali kuwa sikivu baada ya kuwasilisha kero hiyo na kuikumbushia wakati wa  Bunge sasa utekelezaji umeanza. Pia ameishukuru Serikali kutoa takribani Shilingi Bilioni kumi kwaajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maji Jimboni humo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani wa Kata za Shambarai burka na Mbuguni wameishukuru serikali kwa mradi wa urejeshaji maji ya mto nduruma kwenye mkondo wake kwani ilikuwa ni changamoto ya wananchi wa Kata hizo kwa muda mrefu.

Nao wananchi wa Kata ya Shambarai Burka wamesema msimu wa mvua wanafunzi walishindwa kuhudhuria masomo kutokana na mafuriko hivyo wanaishukuru serikali kwani mradi ukikamilika utasaidia kudhibiti mafuriko " kunawakati tunashindwa kufanya shughuli za kiuchumi hata miezi 3 kutokana na kukatika kwa mawasiliano kwani barabara zinajaa maji "amesema Neema Mungure mkazi wa shambarai burka.

Uzinduzi huo wa mradi wa urejeshaji mto  nduruma umehudhuriwa na Mhe.Waziri wa Maji,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Kamati ya Ulinzi na Usalama ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Meru ,Wahe.Madiwani wa Kata ya Shambarai, Mbuguni,na Kikwe , Katibu wa CCM Meru na Viongozi wengine wa Chama,Viongozi na Watumishi wa Bonde la Pangani pamoja na Wananchi wa Kata za Mbuguni na Shambarai.




Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa