Wenyeviti wa vijiji 4, wenyeviti wa vitongoji 14 ambavyo ni Kidire , Kwa Filipo B, Ngyeku kati,Maziwa,Kwa Petro, Mamuna,Dipu,Kwakitenga,Saunyi,Nkoanaya,Tengeru,Mbolele,Nkoanekoli,Mwakeny,Kwa Petro, wajumbe wa serikali za vijiji 28 wakiwa ni 16 toka kijiji Maweni na wajumbe 12 toka kijiji cha Ngongongare watokanao na chama cha Mapinduzi (CCM) Wameapishwa leo tarehe 23 Juni 2017 baada ya kuibuka washindi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki wa wenyeviti wa vijiji na vitongoji uliofanyika tarehe 11 Juni2017
Wenyeviti hao wa vijiji Nkoasenga, Ngongongare , Maweni, Patanumbe,wenyeviti wa vitongoji pamoja na wajumbe wa serikali za vijiji wameongozwa na mwanasheria Prosper Ndomba kula kiapo hicho katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,naye afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Meru Edward Chitete amewasisitiza viongozi hao kutekeleza majukumu yako kwa kuzingatia sheria
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa