Wenyeviti wa Vijiji ,Wenyeviti wa Vitongoji na Wajumbe wajumbe wa Serikali za Vijiji wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo katika kuwatumikia wananchi ili kuendana na azma ya Mhe Rais Magufuli ya kuwaletea watanzania maendeleo.
Hayo ameeleza Afisa Tarafa ,Tarafa ya Mbuguni Ndg.Abdallah Teni wakati akizungumza na wenyeviti wa mitaa na wajumbe baada ya zoezi la kuwaapisha kufanyika.
Teni amesema wenyeviti wa Vijiji ,Wenyeviti wa Vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji ndio viongozi ambao wanakutana na wananchi na kugundua changamoto zao hivyo wanapaswa kushughulika na mambo ya wananchi waliokuchagua bila kujali itikadi za vyama na Dini zao.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Jonathan Kiama amewapongeza viongozi hao kuaminiwa na kuchaguliwa na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, hasa kuepuka kuingilia majukumu ya kisheria ya vyombo vingine.
Afisa Takukuru, Hadija Mhamedi ametoa wito kwa viongozi hao kuepuka kupokea au kutoa rushwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao kwani rusha ni adui wa haki na kwakua cheo ni dhamana ni vyema Viongozi hao wakatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kanuni nataratibu.
jumla ya Viongozi 533 wa Tarafa ya Mbuguni kutoka kata ya Majengo,Shambarai Burka ,Mbuguni na makipa wameongozwa kula kiapo chauaminifu na uadilifu na Hakimu Mkazi Mahaka ya Mwanzo Nduruma, Isile A. Saiba kiapo hiki ni mara baada ya viongozi hao kushinda uchaguzi uliofanyika Novemva 24 mwaka huu ambapo viongozi wote hao wanatokana na Chama cha Mapinduzi.
Afisa Tarafa ,Tarafa ya Mbuguni Ndg.Abdallah Teni wakati akizungumza na wenyeviti wa mitaa na wajumbe baada ya zoezi la kuwaapisha kufanyika.
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Jonathan Kiama
Hakimu Mkazi Mahaka ya Mwanzo Nduruma, Isile A. Saiba kiapo
Afisa Takukuru, Hadija Mhamedi
Picha zifuatazo ni za Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji na wajumbe wa Serikali za vijiji wakila kiapo cha uaminifu na uadilifu
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa