Maadhimisho ya Wiki ya mazingira yanaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo siku 3, wananchi, watumishi wa Halmashauri na wadau wa mazingira wamefanya matembezi ya kukagua uwepo wa mimea vamizi (Invasive species) kutoka Makao makuu ya Halmashauri hiyo hadi geti la kwanza la hifadhi ya Taifa ya Arusha ANAPA .
Akizungumza baada ya kubaini uwepo wa mmea vamizi uitwao gugu karoti Mtafiti Bi Neema Mtenga kutoka Taasisi ya CHANGE FOR FUTURE amesema kemikali zinazotolewa na mmea huo husababisha aleji ya mfumo wa hewa(respiratory difficulties) pia hutengeneza sumu kwenye mwili wa binadamu hivyo husababisha vipelevipele (contact dermatitis) na endapo mnyama akila mmea huu kwa 50% ya chakula inapelekea mnyama kufa au maziwa na nyama kubadilika ladha au kutokuwa naladha.
Naye ,Bw.Praygod Kweka kutoka Chuo cha NELSON MANDELA amesema mme huo unamadhara Kwenye mazingira kwani husababisha kupotea kwa bioanuai(biodiversity loss) pamoja na kubadilisha uoto wa asili. Pia Kwa sababu mmea huo hutoa kemikali zinazo zuia mimea mingine iliyo karibu kumea hivyo hupelekea kupunguza uzalishaji (reduction in crop yield)
Pamoja na kupoteza mfumo wa udongo (soil properties )
Awali, Mtafiti Neema
amesema mpaka sasa njia mbalimbali za kuangamiza gugu karoti zilijaribiwa bila mafanikio kwa asilimia 100% hivyo njia pekee ya kuangamiza mmea huo ni kung'oa kabla halijatoa maua au mbegu na mtu anapo ling'oa ahakikishe anavaa mfuko wa nailoni au cloves ilikuepuka madhara kwenye ngozi.
Aidha , Bi.Damar Nassari kutoka hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA) amesema jitahada zaidi za kudhibiti mmea huo zinaitajika kwani mmea huo ukiingia hifadhini unaweza kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuathiri uoto wa asili wa hifadhi hivyo wanyama pori kukosa malisho ya kutosha ndani ya hifadhi .
Mkurugenzi mtendaji anapenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki siku ya tatu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira ikiwa ni pamoja na Chuo kikuu cha Nelson Mandela, ANAPA, Change for future, Dunia Salama Foundation, Twice Foundation, Awe College, Twice Foundation na Ngarasero Mountain lodge.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa