Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango ametoa wito kwa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu kwenye kampeni ya siku nne ya awamu ya tatu ya utoaji chanjo ya matone ya Polio kwa Watoto wenye umri chini ya Miaka 5 (0 -5) ili kuzuia ulemavu wa viungo unaosababishwa na ugonjwa wa Polio.
Akizungumza katika kikao cha uhamasishaji wa chanjo ya polio Halmashauri ya Meru, Mhe.Ruyango amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa chanjo na bajeti ya utekelezaji wa wa awamu ya tatu ya utoaji chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio ili kuhakikisha watoto wote wa Kitanzania wenye umri chini ya miaka mitano wanakuwa Salama kwa kupata chanjo hiyo kwani ugonjwa wa Polio umeripotiwa katika nchi jirani ya Malawi .
Vilevile Mhe. Ruyango ameipongeza Halmashauri ya Meru kufanya vizuri katika utoaji wa chanjo hiyo awamu ya pili ambapo ilivuka lengo kwa asilimia 138% na kuwataka wataalum kuhakikisha katika awamu hii ya tatu wanafanya vizuri zaidi kwa watoto wote chini ya miaka mitano kupata chanjo ya Polio " nitoe wito kwa wataalam watakao toa chanjo kuhakikisha wanawafikia watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano " ameagiza Mhe.Ruyango
Mratibu wa chanjo halmashauri ya Meru , Salome Mbegela amesema utoaji wa chanjo ya Polio awamu ya tatu utafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 01 hadi 04 Septemba 2022 ambapo chanjo hiyo ya matone itatolewa kwa watoto wote wenye umri nchini ya miaka mitano nyumba kwa nyumba ,vituo vya kutoa huduma za afya,vituo vya kulelea watoto , katika shule nk
Dkt.Focus Maneno ambaye ni Mkuu wa Idara ya huduma za Afya, Lishe na ustawi wa jamii amesema chanjo ya Polio ni muhimu sana kwani ugonjwa wa polio unasababisha mtoto kupooza na kupata ulemavu wa viungo .
Mshili Mkuu wa Meru Ezron Sumari amesema chanjo ya ugonjwa wa Polio ilikuwa toka miaka ya nyuma hivyo ametoa wito kwa Wananchi wa Meru kutoa ushirikiano katika zoezi la chanjo ya Polio ili watoto wawe salama.
Kwa upande wao Viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho wametoa wito kwa jamii kuhakikisha watoto walengwa wanapata chanjo hiyo muhimu ambapo Mchungaji Exaud Nnko amesema ulemavu na kupooza kwa watoto ni janga la jamii nzima hivyo jamii haina budi kuzuia janga hilo kwa kuhakikisha watoto chini ya miaka mitano wanapata chanjo.
Aidha, watoto elfu 56,591 wenye umri chini ya miaka 5 wanatarajia kupata chanjo hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango wakati wa kikao
Mshili Mkuu wa Meru Ezron Sumari wakati wa kikao
Wadau wakati wa kikao
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa