Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela amekipongeza kikundi cha Vijana TAZAMA kilichopo kata ya Akheri Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa namna vijana hao wamejiunga na kuanzisha miradi kwa lengo la kujipatia kipato.
Aidha Mhe.Mongela ametoa wito kwa maafisa maendeleo ya Jamii kutumia vikundi vya vijana vinavyofanya vizuri kuwaelimisha vijana wengine kwa uhalisia " msiwasafirishe vijana kwenda Mikoani kujifunza watumie hawa wanaofanya vizuri kuwaelimisha wengine "amehimiza Mhe.Mongela.
Godlisten Mbise ambaye ni kijana wa Kikundi cha TAZAMA ameishukuru Serikali kwani wamekuwa wakiwa wakipata ushauri wa kitaalam ambao umekuwa na tija katika utekelezaji wa miradi yenye thamani ya zaidi ya Milioni 28 ya ufugaji wa Ng'ombe wa Maziwa 8, ufugaji wa Mitambaa 5 na utotoleshaji wa vifaranga .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya amesema kikundi cha Vijana TAZAMA ni miongoni mwa vikundi ambavyo vitanufaika na mkopo usio na riba wa asilimia 10% ya makusanyo ya Halmashauri .
Aidha,Mwl.Makwinya ametoa wito kwa Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuchangamkia fursa ya Mkopo usio na riba unaotolewa na Halmashauri kwani kumekuwa na mwamko mdogo wa vikundi vya vijana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa